Return To Message Board
Author Topic:   ASKOFU MOSES KULOLA KADA WA CCM?
MUNISHI
(Moderator)
posted 2/27/04 2:38 PM    
CCM tangu wakati wa Nyerere, ilimpatia Kulola walinzi wanaolipwa na serikali, ili akipigie debe chama hicho. Kulola alikaidi uongozi wa TAG ikazuka vita kati yake na Askofu Emanuel Lazaro. Serikali ilimpendelea kulola kwani alidai misaada mingi kutoka Marekani ilikuwa na lengo la kupenyeza CIA Tanzania kwa kutumia TAG. Nyerere aliinunua hiyo jumla kwani sera zake za ujamaa zilizoshindwa zilikuwa zikihofu sana Marekani wasijeleta ubepari Tanzania. Kulola alionekana malaika wakati Lazaro serikali ilimuona shetani. Lazaro alikwamishwa mpaka alipoachia ngazi ya uaskofu. Kulola mpaka leo anafaidi uongo wake wa kuidanganya serikali kwamba CIA walimtumia Lazaro. Ukiyasikiliza mahubiri ya kulola kwa makini, utakuta anawalisha waumini siasa za CCM bila wao kujua. Kulola ndiye mhubiri wa DOLA Tanzania. Mikutano yake inalindwa na kikosi maalum, Yeye mwenyewe analindwa kila aendako, Ni kipenzi cha CCM. Tuombe iwe hata mbinguni Mungu atampa heshima anayopewa na CCM. Vinginevyo atakuwa ameshavuna duniani. Nchini Kenya Kitonga aliipamba sana KANU na alikuwa mhubiri wa dola Kenya. Tangu KANU waachie ngazi Kitonga yuko nje ya duara la madaraka.


http://munishi.com
http://munishi.com
MAIKO posted 3/19/04 12:13 AM    
Ndugu Munishi. Bwana Yesu asifiwe saaana. Nashukuru kwamba umeliona hilo. Wengi tumekuwa tukishangazwa na mahubiri ya Kulola. Kwani kila mwaka mahubiri ni yale yale. Utafikiri hakuna kinachotokea na hasa Tanzania.
Nakubaliana nawe kwamba huyu mzee ni KADA wa CCM. Mwanzo nilifikiri ni mimi mwenyewe ninayetilia mashaka mahubiri ya Kulola. Nimeshukuru kwamba roho wa Mungu amekupa ujasiri kuliweka hili wazi. Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu Munishi.
Mkereketwa posted 3/30/04 9:53 AM    
Jamani naona mambo sasa ni mazuri. Kwamba hata matapeli wa kidini wanawekwa wazi hiyo ni hatua nzuri.Mwenyewe shutuma zangu kwa Mwinjilisti Moses Kulola, ni kuhusu jinsi anavyowapambanisha vijana kuoana bila wenyewe kufahamiana kwanza.Umekuwa mtindo wa miaka mingi kwa wasichana wanaotaka kuolewa kumwendea Kulola na kumweleza hitaji lao hilo. Naye Kulola huahidi kuwaombea. Kwenye mikutano yake huwahimiza vijana wa kiume waoe lakini huku akiwachagulia wachumba katika listi yake ndefu.Matokeo ni kwamba ndoa hizo hazidumu. Kanisa huandaa kila kitu kwa ajili ya arusi, lakini wakishaoana wanaachwa peke yao wapambane na maisha. Mambo yanawawia magumu kwani kwanza hawajuani, hawakupendana, bali walitii amri ya Askofu wao kuoana.Kwangu mimi huo ni upotoshaji wa hali ya juu. Na kulola anapaswa kuambiwa kwamba aache kuwachagulia watu wachumba.Mfano wa Ndoa alizopambanisha Kulola na sasa zimevunjika ni ndoa ya MZUNGU FOUR Na JESKA. Mzungu anadai hakuwahi kumpenda Jeska, lakini ilitokea kwamba Jeska alikuwa katika listi ya wale waliokuwa wakitaka kuolewa, na Kulola alimlazimisha Mzungu kumuoa Jeska.Kanisa la Mnazi mmoja liligharamia kila kitu cha maharusi mpaka mavazi.Ilipofika zamu ya MZUNGU FOUR na Jeska kuishi kama mke na mume, yakawashinda na sasa ndoa yao imevunjika.Pia mtoto wa kike wa kulola aliwahi kulazimishiwa kijana waoana, yakawashinda na Kulola mwenyewe aliwatalikisha na kumwoza msichana wake kwa kijana mwingine. Hatujui kama bado wanaishi pamoja lakini ndoa nyingi katika Kanisa la Kulola ni kichekesho.Kama zinaendelea lazima kila kitu hata m,apenzi kati ya mke na mume wapate ushauri kwa Kulola.Kwangu naona kwamba Mzee kulola hawezi kuhusika na kila ndoa kanisani mwake na huo ni upotovu unaotakiwa kukomeshwa mara moja.
Mapunda S. posted 4/16/04 8:01 AM     Click here to send email to Mapunda S.  
Mimi nilifikiri kuwa Munishi ni mlokole mzuri, kumbe ni mchanga sana kiroho..Tangu sasa naenda choma mikanda yako yote ya nyimbo zako! Ndio maana sikuwa nikibarikiwa na nyimbo zako! kwa maana hazina nguvu ile ya Roho Mtakatifu.. Badala ya kuzungumzia mambo ya maana, unazungumzia mambo ya upuuzi. Je kweli wewe umeokoka?


http://www.netsoltz.com
Munishi
(Moderator)
posted 4/26/04 12:34 AM    
Mapunda Mimi nimeokoka tena nimejazwa na roho Mtakatifu. Hiyo haina maana nitawazuia watu kutoa madukuduku yao hapa hata kama yanamlenga KULOLA.Kanisa ni mwili wa Kristo ambao unafaa kujengwa na kulindwa usiingie dosari. Kanda zangu hujawahi kuwa nazo, kwa hiyo sijui utaenda kuchoma nini. Ila unaweza kusikiliza hapa http://munishi.com/redioinjili.htm


http://munishi.com
Gazeti Injili Online
Maiko
(Moderator)
posted 4/26/04 12:52 AM    
Kwani Kulola ni nani? Siyo mwanadamu mwenye udhaifu kama wengine? Akionyeshwa udhaifu wake kuna kosa gani? Kweli Kulola ahubiri Injili bali anawapendeza wanadamu hasa CCM na viongozi wake.Anatimiza maandiko kwamba siku za mwisho watu watajipenda wenyewe kuliko Mungu.Kulola afurahie heshima anayopewa na CCM na ajue mbinguni haingii. Siyo kwamba ninamhukumu, lakini hawezi kutuhubiria porojo badala ya injili halafu afikiri kwamba ataingia mbinguni. Ana wakati wa kutubu na asipofanya hivyo ole wake.


http://munishi.com
Gazeti Injili Online
MWANGOMOLA posted 4/26/04 3:30 PM    
jamani mwacheni mtumishi wa Mungu MUNISHI atueleze ayajuayo kumhusu Kulola. Waliwahi kuzunguka pamoja kuhubiri injili. Sisi wengine tunaweza tusimjue Kulola kwa kina lakini Munishi anamjua.Siungi mkono tuhuma ambazo hazina msingi, lakini hizi za Kulola naona zina msingi kabisa. WANAOMCHUKIA MTUMISHI WA MUNGU MUNISHI WANA HAKI YA KUFANYA HIVYO. LAKINI WASIMZUIE KUSEMA KWELI KUHUSU KULOLA. HAPO WATAKUWA WAMETUKOSEA SANA.
joy posted 5/18/04 12:15 AM     Click here to send email to joy  
jamani Kulola alikuwa anafikia nyumbani kwangu wakati anahubiri Injili kwenye mji fulani hapa Tanzania - mbona sikuona hao walinzi wa serikali waliokuwa wanamlinda?? jamani mwacheni mtumishi wa Mungu kwani hata nyie mnaomlaumu mna madhaifu yenu tele - hebu tusubiri kwani wote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu aliye hai. Isitoshe kuliko kumlaumu na kumwandika si bora kumwendea na kumweleza??? Nashangaa mtu kusema eti kila mwaka mahubiri yake ni yale yale - NGUVU ZA MUNGU hazishuki kwa kubadilisha ujumbe ila hata kama ujumbe ni huo huo miaka yote mradi YESU anahubiriwa, watu wanaokoka na YESU anahudumia watu. ACHENI WIVU mwenzenu tangu aanze huduma ameleta maelfu kwa YESU - HEBU FIKIRINI KUFANYA NA KUANDIKA MAMENO YENYE BARAKA YATAKAYOMFAA MWENYE KUSOMA AU KUSIKIA. MUNGU AWASAMEHE SANA KWA KUMSHUTUMU MTAKATIFU WA MUNGU MZEE KULOLA.
Maabadi posted 5/29/04 6:13 AM     Click here to send email to Maabadi  
Ndugu zangu, mimi si msomaji hasa wa mtandao huu, lakini haya mnayoyajadili hapa hayapaswi kufumbiwa macho. Napenda kuanza na Ndugu Munishi ambaye nimesikiliza nyimbo zake tangu wakati nilipozaliwa mara ya pili mnamo mwaka 1990. Hizi hoja za kuwachambua watumishi wa Mungu haziujengi mwili wa Kristo hata kidogo, nilitegemea kwamba yeyote ambaye angeanzisha website ya namna hii angefanya kila linalowezekana kuwaleta watu kwa Yesu na si vinginevyo unless unatumiwa na devil! Mimi si muumini wa madhehebu ya Kulola wala Lazaro wala CCM wala Mrema! bali ni mkereketwa wa damu iliyonisafisha ya Yesu Kristo, na hapa Marekani ninakoishi ninaabudu katika Non-denomination church huku nikimtumikia Mungu kadri anavyoniwezesha. Kulola nimemfahamu tangu utoto wangu na sikuwahi kuwa na interest yoyote ya maisha yake binafsi ila nilichokiona madhabahuni ndicho roho yangu ilichokihitaji na si vinginevyo! si busara kumkosoa mtumishi wa Mungu ambaye kila siku na katika maisha yake yote amekuwa akipiga kelele za kuwavuta watu kwa Yesu! yawezekana wengi wetu ni matunda ya huduma yake ukiwemo wewe Munishi! lakini wajibu wangu kama mkristo ni kuwaheshimu walionifikisha hapa nilipo na kuheshimu huduma zao nikiwaombea kwa bidii na si kutumia mifarakano binafsi katika kuizorotesha kazi ya Mungu. Hivi ndugu Munishi hukumbuki biblia inaposema u nani wewe uhukumuye? kwa nini usimsubiri Mungu ahukumu ambaye atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake? na hiyo CCM na Nyerere vimekukosea nini? mbona tulipokuwa tunajenga nchi wewe ulikimbilia Kenya? hebu kaa chini na utubu ili uanze upya utumishi usiochanganyika na takataka!
Adeline Siame posted 6/2/04 12:55 AM     Click here to send email to Adeline Siame  
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Munishi sijui watu waongee lugha gani utakayosikia wewe, iwe kichagga au kikikuyu kwa kuwa lugha ya kiswahili huielewi kabisa. Munishi, wewe ulianzia kazi ya kubeba mfuko wa mzee Kolola, na huyu mzee ndiye aliekufanya wewe hata ukamjua Bw. Yesu Kristo, kwa kuwa karibu nae, mbona huna shukrani, mbona humuogopi Mungu. Kwanini unawachukia watu watu waliokufanya wewe ukajulikana? Mbona huwapendi wazee kuanzia baba wa Taifa hili hadi wachunga kondoo wa Bw. Yesu Kristo wote unawachukia, je wewe umefanya maendeleo gani hata Mtanzania/Mkenya alieko huko vijijini akakubariki. Kwa nini usitumie hiki chombo tulichopewa kama zawadi kutoka mbunguni kwa ajili ya kuwaelimisha watu ili wamjue Mungu? Kwa nini usituandikie misitari ya Biblia takatifu tukasoma badala ya utaratibu huu wa kulumbana kisiasa au kidini, kweli kwa njia hii Munishi ukifa leo utafika mbinguni au utakuwa umepoteza muda wako bure, wape watu wenye busara hii website ili wawalishe watu neno la Mungu, watu wengi wana kiu ya kujua mambo mazuri ya ufalme wa mbinguni, sio kuwajadili watu, je utakataa ukiitwa wewe ni baba unaefahamu mambo mengi lakini ni mchoyo kwa kuwa unawadanganya watu waunge mkono mambo yako ya kijinga? Munishi wewe natumaini husomi biblia takatifu, na kama unasoma roho wa bwana hayupo kwako, omba sasa, tubu, waombe msamaha watumishi wa Mungu uliowakashifu,je hujui ukifungiwa hapa duniani hata mbinguni utakuwa umefungiwa. Tulishe neno la Mungu achana na malumbano, unatupotosha kaka.
Spear Mbilinyi posted 6/9/04 8:32 PM     Click here to send email to Spear Mbilinyi  
Hello, I'm not that "a person of faith", but I do live with things and knowledge that come through empirical evidence. I'm that very critical to people who think they are better and at most can judge other people.I've read and clearly noticed that many of Munish political article and interests are shallow, and therefore desired attention. MUNISHI is a wrong Moron, He is, and has been unable to show any political understanding that transcends to political leadership.His I.Q is of 18 years old boy or of very old person, His L.Q is very minimum to think of becoming a president just listNina Miaka 25, lakini Munishi hawezi kuniongoza, kwani uwezo wake wa kufikiria ni mdogo sana, Angalia mtu ambaye analalamika bila kuwa na "analysed information", kwa mfano, articles zake nyingi anamlaumu kila mtu, kwanza Nyerere na Pili...tatu... na sasa anamlaumu KULOLA (Simjui kulola ni nani). halafu ana'Link' information na CIA. Does this Moron MUNISHI has any evidence to support whatever he says especially when He includes CIA. It is such absurd and ridiculous to have someone who think of Tanzanian Presidency to have that shallow understanding on the standard ethics.MUNISHI is also a person so weak to personal favors, you can see this attitude when put close analysis to questions he has been asked, for example one individual in the forum express that "I will dump his cassettes" He came up in stead of logic answer boasting on "I have them at http://...."All these are BULL-SHIT low level I.Q, Munishi knows to sing... therefore He should do the thing He knows Best... TO SING. The moment He shows up in the politics, in these days we eliminate HIM..especially to the person with little education."Before thinking of Big things, One need to examine principles through a critical thinking and in depth analysis, Going action need strategic planning"


http://www.hbs.edu/doctoral/
mpendwa posted 6/18/04 3:34 PM     Click here to send email to mpendwa  
Bwana YESU asifiwe MPENDWA MUNISHI kwa kweli tunakushangaa hatujategemea mtu kama wewe kuzungumza mambo kama haya unatusikitisha sana mpendwa kwani badala ya kutufundisha mambo ya mungu ukiwa kama mtumishi wa mungu unaingia kwenye ulingo wa siasa na kuanza kumkandia mtumishi wa mungu alichaguliwa na kuheshimiwa na mungu sio kwamba ninamtetea bali hukupaswa kutoa kashifa zako kwa watu bali ungemfuata yeye binafsi na kuzungumzia swala hili au tafuta email yake Kama mtu wa mungu unatakiwa umuombee na kutumia hekima kutatua tatizo hilo sisi kama wapendwa tunaona una lako jambo tena tukizingatia kwamba una gombea urais huoni kama unajipigia debe kiaina kwa kuikandia ccm haifai hivyo mpendwa onyesha mfano bora kama mkristo unaye mpenda mungu kwa kweli ngoja nikueleze mpendwa bora ujiengue mapema kwenye listi ya wagombeaji kwani ninahakika kwamba utaaibika kwani hata wewe umemuaibisha mtumishi wa mungu lakini pamoja na hayo yote sisi tunakuombea mungu akubadilishe na urudi kuwa munishi yule wa zamani aliyekuwa akituburudisha kiroho na kimwili
Munishi posted 7/8/04 3:16 PM    
Kweli duniani kuna MAMBO. Kujadili kuhusu KULOLA ni dhambi? Poleni sana.Nawaombea Watanzania wenzangu wajue kwamba ni haki yao kuhoji chochote hata kama wanayemjadili ni Baba Mtakatifu, Nyerere, Kulola, NK.Sina lolote kibinafsi mimi na Kulola, Lakini siwezi kuwazuia watu wanaotoa madukuduku yao kumhusu Kulola.Neno la Mungu na Injili ni nini, kama siyo kukosoana na kusaidiana hapa duniani? Kulola akifanya kosa aambiwe. Nyerere aliyekosea, yasemwe. Tutaogopa mpaka lini?
Bruno Bernard posted 8/14/04 1:28 PM     Click here to send email to Bruno Bernard  
Bwana Munishi,najaribu kufuatilia hoja zako na majibu yake kwa wanaozisoma hoja hizo katika foram mbalimbali kwenye `website` hii,naona robo tatu na zaidi wanakupinga kabisa mawazo yako. Hii ni kuonesha kuwa uko nje ya mstari hasa ikizingatiwa kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu. Kutokana na hilo nakupa ushauri kuwa unatakiwa kubadirika na kufuata yale wanayokushauri.`Website` kama hii inatarajiwa kuzungumzia mambo ya Mungu, watu wamjue Yesu anayeokoa na waokoke, si kama haya tunayoyaandika. Mimi binafsi ninapoandika hivi naogopa sana nisije nikawa namkopsea Mungu,lakini kwa sababu roho yangu inauma sana ninapoona mkoroganyo kama huu, ninaona nawajibika kuandika yamkini Roho Mtakatifu atakugusa ukabadilika na kujiuliza kwa nini watu wengi wanakuwa kinyume na mawazo yako.Pamoja na kwamba kila mtu ana msimamo tofauti wa mawazo lakini si katika neno la Mungu. Neno la Mungu hasa kwa watu tuliookoka ambao tunasema tumejazwa Roho Mtakatifu tunatarajiwa kuwa na msimamo mmoja; Kama tunasema Yesu anaokoa, basi wote tutasema hivyo, kama tunasema masengenyo ni dhambi, basi wote tutasema hivyo,mmoja akifanikiwa wote tumefanikiwa, na mmoja akianguka wote tumeanguka;tunamwombea yule aliyeanguka ili wote tusimame. Kama tunakwenda tofauti lazima tujue kuwa katikati yetu kuna adui na si mwingine bali ni ibilisi.Unapoandika habari kama hizi za kuwasengenya watumishi wa Mungu ambazo wao wenyewe hawana habarina pia wewe mwenyewe,huna uhakika nazo, unapaswa kujua kuwa unafanya dhambi ya masengenyo, na wasengenyaji wote hawataurithi ufalme wa Mungu!Unapoandika habari kama hizi za kuwasema wengine je wenyewe wanajua? Tuache masengenyo bwana Munishi, kama wamekukera au unahisi wanaenda kinyume na unavyotarajia, waendee na uwaeleze hayo yanayokukera ukiwa kama mtumishi wa Mungu.Acha moyo wa kiburi kwamba labda wewe unajua zaidi, mwogope Mungu mith.29:23. Kama unataka kuingia katika siasa,jitokeze hadharani eleza nia yako ili watu wajue wazi kama ndg Kakobe alivyofanya nyakati zake, na baadaye akatangaza wazi kuwa ameacha mambo ya siasa na kusema kuwa amerudi kanisani.Malumbano ya kwenye computer wale ambao hawajaokoka wanaposoma habari kama hizi hasa ikizingatiwa kuwa `website` yako inazungumzia pia na mambo ya Mungu, wataufikiriaje wokovu wetu? Bila shaka watasema kwamba hakuna kuokoka duniani kama wanavyosema hata sasa, kwa sababu vipimo vya wokovu hata wale ambao hawajaokoka wanavijua, kwa vile torati imeandikwa ndani ya mioyo yao. Mungu akusaidie ili twende sambamba kuwaleta watu kwa Yesu kwa kuitumia `website` hii,na siyo malumbano ya kisiasa na masengenyo yasiyo na maana. ambayo matokeo yake ni kutupeleka jehanam.Anzisha mijadala kama `Je kunakuokoka duniani`Watu tuliookoka tunapaswa kuwaje mbele ya wasioamini?``Maandiko sehemu fulani yanaposema hivi au vile yalimaanisha nini,n.k. Hayo ndiyo mambo ya kujadili; yatatujenga na pia wengine yatawaokoa! lakini hii yako bwana!!. Hapana!!!.
GODFREY posted 12/20/04 10:49 AM    
Naomba nimmuunge mkono Ndg BERNAD kwa mawazo aliyoyoyatoa kuhusu kuwasakama watumishi wa Mungu kwenye website hii si vizuri hata kidogo na ni utovu wa nidhamu kwa sababu watumimishi wa Mungu hatukuwaita sisi wameitwa na Mungu mwenyewe hivyo tumwachie MUNGU aliyewaita badala ya kuwasakama na kujipatia adhabu kwa kuwasema watumishi wa MUNGU . wengi tumemjua yesu kwa kupitia mtumishi wake Kulola hivyo singeona sababu ya kumsakama zaidi ya kumwombea azidi kuihubiri injili ambayo sisi kwetu imekua ya manufaa makubwa.


http://munishi.com
Tausi posted 3/15/05 1:25 AM    
Munishi napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kama kungekuwa na watanzania kama 25000 kama wewe nchi yetu ingekuwa " people must be free to express their opinions in a democratic society " , yaani watu na akili zao wanaogopa kumkosoa kolola ?I feel so sorry for my fellow Tanzanians.
Happiness posted 6/9/05 2:44 PM    
Nimeokoka ninampenda Yesu, nawe munishi unasema umeokoka! kwa nini unaongea mambo yasiyo na maana, yanayokupotezea muda? huo muda ungeutumia kwa maombi na kuombea dunia nzima.Kuna kitu ulichopungukiwa; nacho ni upendo wa Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu.Tubu mbele za Mungu, omba msamaha kwa wote uliowakashfu,badilika na umrudie Bwanakwa moyo wako wote. Wewe sio jaji na wala sio kazi Yako kuhukumu, hukumu ni ya Mungu tu.Ndugu yako akikosea kama huwezi kumweleza wazi basi nyamaza na umuombee ndipoMungu atakapo kubariki, ni kosa kubwa kuwasimanga watumishi wa Mungu. Sisi wote tu wana wa Mungu kama tutasimangana badala ya kuombeana tutakuwa tunampa nafasi kubwa shetani,naye atakuwa anatucheka, ni aibu kubwa mbele za Mungu.Nina hakika huelewi wala hufahamu kinachoendelea, mambo mengi ya aibu nakutisha yanajitokeza kila leo yaani tupo kabisa katika siku za mwisho; Bwana wetu Yesu yupo mlangoni nawe unawachambua watumishi wa Mungu katika mtandao mambo yasiyo na maana, nakushauri badilika: huu sio wakati wa kucheza. Jenga baraka nzuri ndani ya family yako. Pia ni lazima kuheshimu viongozi wa nchi.
Munishi posted 6/11/05 9:14 AM    
Nimeokoka.Wokovu haumaanishi kuyakumbatia maovu. Ni kinyume chake.Pauloalimwandikia Timotheo akimwambia Kemea Karipia, onya kwa upendo wote. Ukimpenda Kulola utamkemea asiende motoni. Ukimpenda Mkapa, Utamwonya kwa yale yatakayompeleka motoni. Mkapa aliwaua waislamu zaidi ya sabini Zanzibar, Mimi siyo jaji. Lakini najua kwamba kuua ni kosa. Mungu anasema katika amri zake usiue. Mkapa akiua na Kulola amwombee baraka, wote mwenye kuua na mwenye kuomba lao ni moja. Mimi nawaambia watubu. Siwabembelezi maana Yesu si wa kuwabembeleza wauaji na wanaokubaliana nao. Hiyo ndiyo Injili. Hii ya kuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa, siijui, sikuhubiriwa hivyo.
Soni posted 6/14/05 10:23 AM    
Nimesoma kwenye web site ya gospelgtv.com kwamba Kikwete siyo wetu.Wakati Waislamu wameanza kumshuku Kikwete, Wakristo nao wanasema kikwete siyo wao. Magazeti yenye misimamo mikali ya Kiislamu yamemtaka Jakaya Mrisho Kikwete atangaze msimamo. Ama aachane na Uislamu abatizwe awe Mkristo, au abaki Mwislamu. Walihoji kwamba kikwete hawezi kuwa na dini zote mbili. Yaani hawezi kuwa Mwislamu Mkristo. Nao Wakristo kwa upande ule mwingine wanashindwa kabisa kumwamini Kikwete kwani wanajua wazi kwamba yeye ni Mwislamu. Kwa Lugha inayoeleweka, Waislamu wanapomuona Kikwete na maaskofu, wanahisi kwamba huko amepewa nyama ya nguruwe awaletee msikitini. Nao Wakristo wanapomuona Kikwete kanisani kabla ya kubatizwa na kuukana Uislamu, Wanaona kama ametumwa na wenzao walete majini kanisani. Tayari Bwana Kikwete ana kibarua kigumu kuhusu imani yake kwa Mungu. Urais anautaka na Uislamu bado anaupenda. Ujanja wa wanasiasa kuwatapeli watu wa dini unafikia mwisho. Nyerere alifanikiwa kuwadanganya Watanzania kwamba CCM na serikali yake havina dini, Lakini baada ya Mkapa Mkristo kuwaua Waislamu Zanzibar, Watanzania wamejua kumbe serikali na CCM zina dini. Wanapotafuta mpaka wa dini na siasa wanakosa. Kwani wenye dini ndio wapiga kura. Tena kwa CCM kumteua Kikwete Mwislamu baada ya Mkapa Mkristo aliyekuja baada ya Mwinyi Mwislamu, Aliyechaguliwa na Nyerere Mkristo, sasa ni wazi kwamba dini mbili ndizo zinazopokezana uongozi Tanzania. Waumini wa dini nyingine wanaona wananyimwa haki na dini mbili ambazo zimeitawala Tanzania tangu tupate kile walichokiita UHURU. Kwa wale wasio na dini pamoja dini nyingine ambazo siyo Wakristo wala Waislamu, wakati sasa umefika nao wapewe nafasi ya kuiongoza Tanzania. Imegunduliwa kwamba Lugha ya Serikali haina dini ilitumiwa kuwapumbaza Watanzania kumbe kinachotawala ni DINI. Mbona baada ya Nyerere Mkristo alifuata Mwinyi Mwiislamu? Tena mbona baada ya Mwinyi Mwiislamu alifuatiwa na Mkapa Mkristo? Au tuseme yote ni bahati mbaya kwamba baada ya Mkapa, CCM wameona vyema wamteue Mwislamu Kikwete? Kama tutalazimishiwa Kikwete basi duara la Waislamu na Wakristo kuitawala Tanzania sijui litaishia wapi.Tunashangazwa na ukimya wa dini zilizoachwa nje ya uongozi huku wakidanganywa kwamba "Serikali haina DINI. Suluhu ni KATIBA iwaruhusu wagombea binafsi ili kila dini iteue mgombea wake. Magazeti ya kiislamu yana haki ya kujua kama kweli Kikwete wa CCM ni Mwislamu mwenzao. Badala ya magazeti ya Kikristo kuhoji kama Kikwete atalipiza kisasi cha Mkapa kuwaua Waislamu, wao wanapayuka hovyo. Mfano ni gazeti la "Habari Njema" Linalokosoa gazeti la kiislamu.Kikwete wa Jakaya ni uteuzi wa CCM. Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Kwamba CCM wamemteua mtu wao, hiyo siyo sababu tosha kulifanya Gazeti la Kikristo kuanza kupayuka. Mbona? Habari Njema wanasahau kwamba wanasiasa ni WAONGO. Sasa wanalitapeli Kanisa. Badala ya Gazeti la kidini kuwaonya kondoo dhidi ya MBWA MWITU wanasiasa, Wao wanaanza kufurahia posho wanayotupiwa kama KUKU atupiwavyo mahindi kumbe yanaashiria mwisho wake. GTV Tumekataa kumeza ndoano ya CCM hata waweke chambo gani. Tutatumia kila lililo ndani ya uwezo wetu kuwaonya Watanzania wajihadhari na mnyama huyu CCM. Amewameza wenzetu kwa zaidi ya miaka arobaini, na sasa anatutapeli tumwachie nafasi aendelee kutumeza kwa miaka mitano ijayo. Haiwezekani, Hatukubali, Hatutaki, Tena tumekataa.Uhuru wa CCM kumteua Kikwete wa Jakaya, unapaswa kuishia pale uhuru wetu kuteuliwa kama wagombea binafsi unapoanzia. Kuanza kushangilia na kutumia pesa za walipa kodi kununua nafasi kwenye vyombo vya habari ili kutoa kauli za kiburi, Hakutaisaidia CCM. Ikiwa gazeti la kiislamu liliandika kwamba Waislamu hawamtaki Kikwete kwani ni kibaraka wa KANISA, "Habari Njema" Wangepaswa kumkemea Kikwete aache kulitumia Kanisa kwa manufaa yake kisiasa. Akifikiri anajitengenezea mazingara ya kukubaliwa na Wakristo, atajikuta pabaya. Waislamu wameanza tayari kumkana kwamba yeye kikwete si mwenzao. Wakristo nao sidhani kwamba watadanganyika na tabia ya ghafla ya Kikwete kuwa mgeni makanisani. Wengi wameanza kuifananisha tabia hiyo na pipi apewazo mtoto aache kulia. Wanasiasa Tanzania bado wanafikiri kwamba Watanzania ni watu wasioweza kuchambua mambo. Mwislamu Kikwete anapoanza kuingia kwenye majumba ya ibada {MAKANISA} bila kuukana uislamu ni sawa na kuwatania wenye imani hizo. Kifupi niseme "ANAKUFURU." Sambamba na hilo, Mkristo Benjamin Mkapa anapojifanya kuingia misikitini bila kusilimu awe Mwislamu, hiyo ni KUFURU kwa dini ya Kiislamu. Nasema hivyo kwa sababu wote wanajua nini kinapaswa kufanyika ndipo mtu awe muumini wa dini. Kuyakataa masharti ya dini husika na uingie humo ukiwa KAFIRI, kisha utoke humo ukiwa umewadanganya, hiyo inaonyesha kukosa adabu kwa Mungu anayeabudiwa na watu hao. Ikiwa wanasiasa hawawezi kuikosea adabu bendera ya nchi, Vipi wakose adabu kwenye sehemu za kuabudia??? Wanakuja makanisani na ahadi za uongo. Wachungaji na Mashehe wanakubali vipi wanasiasa waingize unajisi Makanisani na Misikitini? Sehemu Takatifu mnakubalije Kikwete aingie na uchafu wake na atoke akiwa amewachafua? Kulingana na imani ya Kikristo Kikwete Mwislamu lazima aukane uislamu ndipo apewe nafasi ya kufanya chochote Kanisani. Mambo ni hivyo hivyo Misikitini. Kafiri hawezi kuruhusiwa kuingia Msikitini akiwa amevalia viatu, huku amebeba nyama ya nguruwe. Hiyo ni KUFURU na kuikosea adabu KORAN TUKUFU. Wanasiasa wanapoingia Misikitini kwa lengo la kuwadanganya Waislamu wawaunge mkono, ni sawa na kuingia na nguruwe msikitini. Wanakuja na pesa za Rushwa na wanawanunua wakuu wa dini. Hilo ni kosa linalopaswa kukemewa na magazeti yote ya kidini. Tunalishangaa "Habari Njema" Gazeti la Kikristo kuanza kumpigia Debe Kikwete wa Jakaya na kusema ni wa wote. Wangefanya vizuri kusahihisha hilo na kusema Kikwete ni wa Jakaya na tena wa CCM. Watanzania wana mtu wao.Tunachoomba ni kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kumchagua yule watakaeona anawafaa kuwaongoza. Kujaribu kuwalazimishia Kikwete, msishangae akiwa kiwete kama Mkapa. Nyerere alitulazimishia Mkapa, akatoka akiwa kiwete, Mkapa asijaribu kutulazimishia Kikwete kwani Mungu anajua nini cha kufanya na wale wanaowatesa Watanzania. Sina tatizo na uteuzi wa CCM, lakini namuomba Bwana Kikwete asije Kanisani kwangu kututapeli kwamba yeye anatupenda Wakristo. Ikiwa anaupenda kweli Ukristo, Kipimo chake ni aikubali Injili ya Yesu, Kisha amwamini Yesu badala ya Mtume Mohamad, Halafu tumbatize aitwe jina lolote hata kama akipenda kubaki na jina lake Kikwete hatuna tatizo hapo. Akikubali hayo tunamkaribisha kanisani. Lakini siyo aje kutuletea pesa za wizi.Huku akijifanya anachangia miradi ya dini ya Kikristo. Gospel TV tunaunga mkono gazeti lililomkosoa Kikwete na kusema kwamba Waislamu wamemshitukia Kikwete. Nasi GTV tunasema kwamba hata Wakristo wa kweli, Tumemshitukia Kikwete. Labda ajaribu mbinu nyingine. Lakini hii ya kuja Kanisani mwenye dhambi halafu aondoke ametuingiza dhambini tumeikataa sawa na tulivyomkataa shetani na mambo yake yote.Tunajua wazi kwamba Kikwete na kanisa sasa watakuwa kama pete na kidole. Lakini kwa muda gani? Wanasiasa huwaadaa watu wa dini wanapotafuta kura. Lugha kama Kikwete ni wa wote hazitaisha midomoni wakati wa uchaguzi. Unafiki huu tunataka ukome. Uongozi siyo kuikana dini. Inawezekana mtu akawa kiongozi bila kuikana dini yake. Ukija kanisani kwa kuwa unataka kuchaguliwa, huo ni UNAFIKI. Kama kweli ulikuwa mtu wa dini zote, basi tungekuona kanisani tangu mwanzo na siyo wakati wa uchaguzi. Hivi wanasiasa wanamdanganya nani? Mungu au wanadamu? Watu wa dini wakiwakosoa wanasiasa wanaowaua watu bila sababu, wanaambiwa wasichanganye dini na siasa. Kwa maneno mengine, Mkapa Mkristo ana uhuru wa kuwaua waislamu Zanzibar, na asiulizwe chochote na waislamu wala Wakristo. Eti wakiuliza, wanachanganya dini na siasa. Mgombea urais akiwa Mkristo, Ataanza kuwatapeli waislamu kwa kujifanya anachangia miradi ya maendeleo misikitini. Akishachaguliwa mambo yanakuwa kinyume. Mfano mzuri ni Mkapa. Alipokuwa akiomba kura, alisema yeye ni Rais wa wote. Alipochaguliwa alianza kuwabagua Waislamu. Aliungana na Amerika kuamini kwamba kila Mwislamu ni Ghaidi. Ikawa kupata hati ya kusafiria ukiwa Mwislamu ni sawa na ndoto. Hayo yote yanafanyika chini chini, huku Mkapa akihubiri kwamba yeye ni Rais wa waislamu na Wakristo. Huu ni unafiki tunaotaka ufike kikomo. Ikafika siku ya siku. Ndugu zetu Zanzibar wakatumia haki yao ya kikatiba kusema kwamba hawaitaki CCM. Mkapa Rais Mkristo, akaamuru Waislamu zaidi ya sabini wauawe, na wengine wakakatwa viungo vyao ili kuwafundisha adabu. Wakristo wenye mtazamo kama wa gazeti la Habari Njema wakashangilia. Walichosahau ni kwamba wanasiasa katika kulinda maslahi yao wanaweza kuua yeyote. Munishi Mkristo niliposema kwamba si haki Mkapa kuwaua Waislamu, Kanda zangu zilipigwa marufuku Tanzania, Mkapa Huyo huyo Mkristo, akaamuru nikamatwe, na Polisi Tanzania wakatangaza kwamba wananisaka. Rais Mkristo anamtafuta Mchungaji Mkristo amuue kwani Mchungaji alimkemea alipowaua Waislamu. Hiyo ndiyo siasa. CCM na huyo waliyemteua wawadanganye wengine lakini GTV Hatudanganyiki na unafiki wao.Kinachotushangaza zaidi ni kwamba wakati wa KAMPENI ni bado. Tena uchaguzi ni bado. Isitoshe vyama vingine havijatangaza wagombea wao. Gazeti la dini limeanza KUPAYUKA. Serikali nayo inafurahishwa na habari hizo. Ikiwa kanda za Munishi zilifungiwa kwa kusema Mkapa ni MUUAJI, Vipi gazeti la Habari njema halijafungiwa kwa kusema kwamba Kikwete ni wa watu wote? Si hapo pia wamechanganya siasa na dini? Ikiwa mnapokea SIFA, Mbona maonyo mnayafungia nje? Ni unafiki huu ndio ulionifikisha mahali pa kusema, "Siasa ni uongo, na kwamba wakati umefika kwa watu wa dini zote kujitenga na siasa. Kila dini ianze harakati za kujikomboa kutoka minyororo ya wanasiasa. Tutafanikiwa hilo kwa kuishinikiza serikali ya CCM kuibadili KATIBA ili iwaruhusu wagombea BINAFSI. Katiba ya sasa inasema mtu hawezi kuwa Rais bila kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa. Nasi tunasema, Huwezi kujiunga na uongo ili uwatoe waongo.Kwani siasa ni uongo.Je Kulola anasemaje kumhusu Kikwete?


http://gospelgtv.com
gospel
ASANALI MSANGI posted 9/11/05 10:35 PM     Click here to send email to ASANALI MSANGI  
Mimi nimeokoka nampenda Yesu kama Bwana na mokozi wangu.Nimeona mengi sana kuhusu Munishi na Kuhusu Kulola,Na wengine wasema watachoma kanda.Mimi nakumbuka mstari mmoja kwenye biblia wasema wengine wanataja magari na farasi lakini "mimi nitalitaja jina la Bwana"Ningeomba wote turudi nyuma nafikiri kuchunguzana kuwa huyu ni mwenye dahambi na mimi sina dhambi haitasaidia kwa maana hautajua siku ya mwenye dhambi atakayo tubu,Na biblia husema aliye wangu namjua na pia huendelea kusema aliyewangu huanguka mara saba na kuamka na kwenda zake.Mambo ya hukumu tumuachie mungu sisi tuhubiri injili tu yatosha na ukihubiri ukumbuke mbegu zingine zitaaguka kwenye miamba,miiba na... na zingine kwenye udongo wenye rutuba.Ndugu zangu ningeona forum hii iwe na lengo la upenda kumbuka Paulo asema 1wakorintho 13:2 Bwana awabariki sana.


http://www.uib.no
Munishi posted 9/19/05 7:01 AM    
Hapo ndugu yangu Msangi umenena.
charles posted 5/9/06 3:50 PM     Click here to send email to charles  
MUNISHI,,,, kama umekosa kitu cha kuhubiri basi nakuomba ujiunge na club ya simba uwe mcheza mpira yaishe. heshimu wazazi wako walio kulea sasa unaongea kwa sababu walikulea, TUBU SASA.
Mosha posted 5/11/06 12:03 AM    
Nani atubu? Kulola au Munishi. Yaani hamuoni ubaya wa Kulola? Uzee siyo tiketi ya kufichiana madhambi. Kama kulola kakosea na Munishi kamkosoa sioni ubaya hapo.Mbinguni hatuingii kwa sababu ya uzee wetu au ujana wetu. Utakatifu ndio tiketi ya kuingia mbinguni. Kulola asipokuwa na utakatifu, kuhubiri na uzee hautamsaidia kuingia Mbinguni. Fungukeni macho ya kiroho muone.
Ocean posted 9/21/06 1:39 PM    
Nimefurahi sana kuona ndugu Munishi amefunguka na kuelewa kiasi cha kujua kwamba kufichua uongo na kuuanika hadharani jambo ambalo biblia inahimiza. Biblia inatuambia tuijaribu kila roho na tuyapime mafundisho yote na kuona kama yanakwenda sawa na neno la Mungu. Pia nasikitika sana kwa ndugu zangu ambao wamedanganywa na kutiwa hofu kiasi kwamba lolote lisemwalo na wachungaji na wainjilisti wanalikubali na kulimeza bila kuyapima kama ni sawa na neno la Mungu.Nimeona pia kwamba watu hawaelewi maana ya Mathayo 7:1-5. Hapa Yesu anasema huwezi kumhukumu mtu anayefanya makosa ambayo na wewe unayafanya. Na kama unataka kumsaidia mwenye kosa tengeneza kwanza mambo yako ndipo uweze kumsaidia vizuri mwenzako aliye kwenye makosa.Naomba wote tukumbuke kwamba maandiko yanaonya juu ya kuzuka kwa manabii na walimu wa uongo ambayo watatujia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo na kudai kuleta mafunuo mapya kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Kwa bila kuwa na watu kama kina Munishi kanisa litalishwa sumu na kupoteza msingi uliwekwa katika neno kupitia Yesu, Manabii na Mitume.Tusione aibu kuwafichua walokole wanatupotosha kwa kuogopa tutaonekana hatuna umoja. Ni afadhali tuonekana hivyo lakini tujenge kanisa lililo na misingi imara katika neno la Mungu.Sasa kuna watu wengi wanaojiita mitume na manabii wanatujia kupitia redio na television na kutulisha maneno yaliyoghoshia na bila ufahamu wakristo wengi tuyapokea na kuyameza bila kuyapima.Naomba tuwe kama Waberoya, tuhakikishe kila kitu tunachofundishwa na kuhubiriwa ni sawa na maandiko na kama kuna kasoro tusikae kimya!!Kumbuka Paulo alimkemea Petro hadharani alipogundua anapindisha mambo kwa kuwaogopa Wayahudi. Na sisi leo tuwafichue na kuwakemea hao wanaotumika kwa hila na uongo.
MUNISHI posted 11/8/06 1:37 PM    
Kuna watu wanaosema nifute yale mabaya yote yanayosemwa kuwahusu watumishi wa Mungu, niache yale mazuri tu. Pengine kwa maoni yao wako sawa. Lakini mimi kama Mhariri siwezi kufanya hivyo. Kwani Kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wa kujieleza. Hatuna hakika kama tuhuma zao ni za kweli au uongo. Lakini kwa sababu nafasi ya kujitetea ipo, wanaoona wameonewa waje wajitetee nasi pia tutachapisha maoni yao bila kutoa hata neno moja. Website ya Injili haipaswi kuandika mambo ya upande mmoja. Ikiwa Biblia yenyewe inaandika habari za shetani akimjaribu Yesu, mbona unataka website ya Injili iandike yale mazuri ya Kulola na Kakobe na siyo yale mengine kama yapo? Hatuungi mkono kuharibiana majina bila sababu za msingi, lakini pia hatuwafungi mdomo wenye madukuduku yao wasiyatoe. Kazi ya website hii ni kuhakikisha kanisa la Mungu ni safi. Kama wewe siyo Kulola au Kakobe, kuwatetea unafanya kazi bure. Pengine yale unayofikiri hawakufanya, wanahukumiwa nayo kwani huenda walihusika katika yale wanayotuhumiwa kwayo. Ni mpaka waseme ndipo watu wanapoweza kunyamaza.Wao wanafikiri wasipojibu yataisha. Website siyo kama gazeti la UHURU. Habari ikiandikwa kwenye gazeti la UHURU inaisha siku hiyo hiyo na jioni gazeti hilo litafungia nyama, au kuwekwa msalani watu wachambie. Sivyo habari iliyoandikwa kwenye mtandao. Kadiri unavyoidharau, ndivyo inavyozidi kuwafikia watu wengi. Ushauri wangu kwa Kulola, ni kwamba aandike habari za kukanusha tuhuma hizo haraka. asipofanya hivyo atajilaumu mwenyewe kwani watu wataamini kwamba kweli yeye ni kama yasemwayo hapa. Lisemwalo lipo kama halipo laja. Huo ni msemo tu.
Ninja posted 11/8/06 2:05 PM    
Bwana Munishi umenena. Lakini kadiri ninavyowajua Kulola na Kakobe, sidhani kama kiburi kitawaacha waje hapa wajibu tuhuma. Ni wakuu kuliko Yesu mwenyewe. Kabla uwaone utakutana na askari wenye bunduki ambao ndio walinzi wao. Wanafurahia kuabudiwa na kuwekwa kwenye madaraka ya juu ambayo hawana. Mtu anaweza kusema kwamba wanalindwa ili wale waliowaibia pesa zao wasije kuzidai.Vinginevyo sioni kwa nini mtu anayejiita mtumishi wa Mungu alindwe na bunduki.
Kamau posted 11/9/06 11:50 AM    
Bwana Yesu asifiwe sana. Mimi ni Mkenya ninayeishi Amerika. Nimesoma kwa masikikitiko jinsi Watanzania wanaoishi hapa Amerika wanavyomtetea Kulola. The Guy was here, and what he did was asking money for nothing. To me Kulola is not a preacher but a cult leader. He preaches to make himself very special man of God of which he is not. Lakini manzee, nilishangazwa kuwaona wabongo wanaofanya kazi duni hapa Amerika wakitoa dola zao eti kumlipia Kulola tiketi ya kuja na kurudi Tanzania. Wengine wanaosha vyombo hapa, lakini walitapeliwa kiasi cha kushindwa kulipa bill zao. Huo ni ujinga.Kwani kuwa mkristo huwezi kusoma neno la Mungu ukalielewa mwenyewe? Ni mpaka Kulola aje Amerika alie machozi ya kuwadanganya ndipo mumpatie dola mlizozipata kwa kuwaosha wazee wa Kiamerika? It is not bad to give, but make shure you pay your bill first. Some preachers will promise blessings wich will not come. To me Munishi is right.
Munishi posted 11/9/06 3:40 PM    
Sasa kijiwe kimeiva.Suala siyo kama tunaweza kumjadili Kulola, ila tunamjadili.Wengine wanasema kwamba Kulola huwachagulia vijana wachumba.Kama kweli kuokoka ni wendawazimu unaomfanya mtu asiwe na uwezo wa kumchagua mwenzi wake maishani, basi hata mimi nisingekuwa nimeokoka. Lakini nijuavyo ni kwamba wote waliompokea Yesu wanapewa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu. Hawapewi uwezo wa kufanyika mazuzu ambayo hata hayawezi kujiamulia chochote maishani. Wanaotaka kuendelea kuwa mazuzu, waendelee wakijua huo siyo wokovu. Yaani wokovu hauondoi uwezo wako wa kuhoji mambo. Ni haki yako. Tatizo la wahubiri wengi, hawataki watu waujue ukweli. Ndiyo maana ni rahisi kuwaambia watu watoe pesa kwa mhubiri, halafu wangojee baraka kutoka kwa Mungu ambaye hawezi kumbariki mchungaji moja kwa moja. Kama siyo kiini macho ni nini? Tukisema mnatuita majina. Basi mnaotaka kuendelea kudanganywa toeni wake zenu kwa wahubiri, kisha pesa zenu zote wapeni, halafu mngoje Mungu awabariki. Kwa ndugu zetu wanaoisha Marekani nimesikia maisha huko siyo mchezo.Hebu wajaribu kukaa juma moja bila kufanya kazi waone jinsi maisha yatakavyowaendea mrama.Biblia inasema kwamba waamini wawe na hekima.Yaani wataifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru mbali na wahubiri MATAPELI.
BABU posted 11/17/06 12:07 AM    
Kweli Munishi ana hoja hapa.Uvivu wetu Wakristo kuwajibika umetuponza. Badala ya kuomba tunaombewa.Hatusomi neno la Mungu tunasomewa.Tafsiri inapopotoshwa wa kujilaumu ni sisi.Matapeli hawawezi kuwepo bila wa kutapeliwa.Wakristo Munishi anaojaribu kuwatetea hawana tofauti na Wahubiri matapeli.Wanaishi maisha nusu kwa shetani na nusu kwa Mungu. Wanahitaji wahubiri matapeli wawaambie yale wanayotaka kusaikia.Kwamba maisha ya utakatifu siyo hoja, mradi tu wametoa.Kwangu wote lao ni moja.Hukumu inawangoja.Ni Ukweli usiopingika kwamba ukimuamini Yesu unapewa uwezo wa kufanyika Mwana wa Mungu. Lakini siyo bila majukumu.Kuomba ni jukumu la kila muamini. Lakini siku hizi imegeuzwa kwamba wahubiri wanawahudumia wakristo kimaombi, tena kwa malipo. Kulola hapendi watu waujue ukweli huu, kwani anafurahi kuwaombea ili wamlipe.Wanaolipa ili waombewe, na wanaoombea ili walipwe, wote wanamtumikia bvaba yao SHETANI. hawana shughuli kujiita watumishi wa Mungu.Ninapompongeza Munishi kwa kazi nzuri, namuomba pia awakemee waumini wavivu wasiopenda kuwajibika.Wajue kwamba hawawezi kununua baraka za Mungu.Pia nimesikiliza wimbo wa Munishi unaozungumzia kwa kina suala hili. Bahati mbaya kaseti inayobeba nyimbo hizo ilipigwa marufuku Tanzania eti kwa kuwa ndani kuna maneno CCM alianzisha Nyerere sasa imezeeka, na sera zake zimeiharibu Tanzania. Kwangu walioizima kanda hiyo, ni maajenti wa shetani. Iwe ni CCM au serikali ya Tanzania, wajifunze kwamba Biblia inamruhusu Shetani mpinzani wa Mungu kutoa maneno au7 maoni yake kwenye Biblia. Vipi CCM wakatae kupingwa? Wazee wazima hata haya hawana? wakiitwa wazee wanakasirika. Wanataka waitwe nini? Kama kweli umezeeka ukiitwa mzee si umeheshimiwa? Mbona CCM walipoitwa hivyo wakakurupuka kama kuku aliyekoswa na mwewe? Mungu atusaidie sana. Awasaidie CCM waache kuwatumia wahubiri walafi na matapeli kama Kulola.Sisi waumini wa KKKT tumeshamshitukia Kulola. Mwanzo aliwatapeli waumini wetu watoke makanisani mwao wajiunge na EAGT. Alipoona mbinu hiyo haizai matunda, alianza mbinu nyingine ya kuwataka waokoke na wakae KKKT mradi tu wachangie mikutano yake ya nje. Swali langu ni hili. Kama siyo utapeli na wizi wa mchana, itakuwaje kanisa la Kulola EAGT lichangiwe na kanisa letu la KKKT? Washirika wake wamchangie.Si walikuwa wakituita hatujaokoka? Tena walisema kwetu tunakunywa kidogo? Mbona kwao wasiokunywa wamegeuzwa masikini kwa michango isiyoisha ya Kulola na watoto wake.Dini ya familia moja itawachangishaje watanzania wote? Mimi ni mlutheri na sitoki kwenda kwa Kulola nikaibiwe.Najua haki zangu. Tena mimi ni mzee wa kanisa KKKT. Nimeokoka na ninaomba siombewi nilipe. Najua kusoma neno la Mungu na roho mtakatifu hunisaidia nilielewe. Sitaki kupigiwa kelele na watu kama kina Kulola na Kakobe.Tena siku hizi amezuka mwingine anaejiita Mtume Mwingira. Msipochunga, huyo Mwingira ataingia mifukoni mwenu na majumbani mwenu, kitakachofuata ni pesa kutoweka mifukoni na wake kutoweka majumbani. Chungeni sana. Siyo kila asemaye BWANA BWANA ni mtumishi wa Mungu. Wengine ni watumishi wa Shetani mwenyewe. Mtawajua kwa matunda yao. Kulola matunda yake ni ndoa zilizovunjika baada ya yeye kuwachagulia vijana wachumba.Ikifikia mhubiri anawachagulia watu wake, nini kingine kitakachofuata kama siyo kuwachagulia wafuasi wake siku ya kufa? Na hayo atayafanya serikali ikimtizama mradi tu awapigie debe CCM izidi kuwa madarakani.Hayo ndiyo nampongeza Munishi kwa kuwa kinyume nayo.
MTOAHOJA posted 2/20/07 6:14 AM    
Mungu asifiwe,Katika jamii ya kidemokrasia, kila mtu ni huru kutoa maoni yake maadam ni ya kimsingi na kuheshimu wenziwao. Mimi ninaona hapa kuna wengine wameshindwa kutoa pointi za kujitetea basi wakabaki kumlaumu Munisi. Kama unapingana na Munisi sio kosa bali toa pointi za misingi kwa nini hukubaliani nae
Edna posted 3/2/07 1:46 PM    
Bwana Yesu asifiwe sana. Katika pita pita yangu kwenye mtandao nimekutana na mada hii na pia, nimeona majibu ya watu wengi waliochangia mada hii,lakini nimesikitika sana kuona kuwa watu wanaacha kazi zao na kuanza kuwasengenya watumishi wa Mungu, kwa sababau hata neno la Mungu linasema tusiwanyoshee vidole watumishi wa Mungu. Na ni hii ni kama kuwanyoshea vidole,na na pia ni usengenyaji ambao hata Mungu hapendi.Kwa nini wewe Munishi kama ni mpakwa mafuta wa Bwana usiwafuate kibinafsi na kuongea nao na kuwaonya? Inakuweje kuiweka hii mada hadharani na kila mtu aseme anavyoona, mimi naona si vizuri kabisa. na unakuwa kama uwahukumu wakati mtoa hukumu ni mmoja tu. Na hata kama wanafanya hivyo usemavyo, kwani wao si binadamu? na unajua binadamu ni dhaifu. Na unaweza kusema kuwa hawajaokoka hawa watumishi wa Mungu, ila inabidi ujue kuwa kuna watu wameokoka na wanampenda Mungu ila kuna roho furani zipo ndani yao. Na watu kama hawa siyo wakukaachini na kuanza kuwahukumu, kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu na unahudumia katika huduma ambayo haikomi, nikimaanisha duniani huduma zote zitakoma ila uimbaji , kumsifu Mungu hakukomi kabisa ungeli sugua magoti na kulia mbele za Mungu ili awafungue katika vifungo walivyofungwa.Mungu akusaidie sana
Luka posted 3/2/07 4:50 PM    
Jamani wakristo wenzangu, inabidi tuombeane badala ya kuhukumiana na kushtumiana mbele ya wana wa ulimwengu, hii ni kumpa nafasi shetani kupanda mbegu za chuki kati yetu. Ndugu Munishi ninakuomba uanze maombi ya kufunga na kuomba ili Mungu akupe roho ya Busara na upendo. Ninaona unaelekea nje ya maagizo ya Bwana Yesu. Kwanini kumhukumu mtumishi wa Mungu Kulola, au kwanini kumuhukumu mtu mwingine yeyote yule na kujenga chuki iliyojificha ndani. Kama hujui hii ni roho ya uhasama na chuki ya ndani kabisa ya moyo wako Munishi, hii ni roho ya Pride . Soma Biblia kuhusu matunda ya roho. Mbona huna upendano wa ndugu wala kiasi (self control?).Munishi ulianza vizuri sana,lakini sasa umeuacha ule upendo wako wa kwanza. Tafadhali fanya maombi ya kufunga na kuomba ili Bwana akuonyeshe mahali ulipouacha upendo wako wa kwanza. Wakati uliokubalika ni sasa. Yesu Kristo anarudi upesi, tafadhali wote tutubu na tuihubiri injili bila majungu wala fitina. Ninawapenda wote. Bwana awabariki sana.
Edna posted 3/5/07 9:29 AM    
Bwana Yesu Asifiwe wapendwa! Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi tena ya kuweza kuandika yale ambayo moyo wangu unanishuhudia. Kwa kweli kitu ninachotaka kusema hapa ni kwamba Ndugu Munishi ufanyavyo si vyema. Wewe utakaa kukazania kuwa oooh! sijui Kulola yuko hivi na hivi mara oooh! atubu. Lakini kumbuka ndugu yangu ya kuwa Yesu yu karibu kuja , na inatupasa tujiandae kikamilifu na kuangalia njia zetu.Hauwezi jua, siajabu Yesu anaweza kuja ukashangaa huyo Kulola na watumishi wengine unaowaona kuwa hawataingia mbinguni wanaenda na wewe unaachwa, inawezekana wakawa wametubu dakika chache tu kabla Yesu hajaja na anapokuja anawakuta washatubu na kuwachukua kwenda mbinguni. Angalia njia zako kwanza kisha waombee na hao unaowahukumu ili Mungu awape neema ya kugundua hayo makosa na kutubu, huo ni Upendo, lakini kuanza kuanzisha mada na kutaka watu wachangie huku ni kukosa upendo kabisa ndugu yangu. Na pia sijui unawafundisha nini watu ambao bado hawaja mjua Kristo Yesu, unadhania wataokoka kweli? Ni bora hii site ungeitengeneza kwa makusudi ya kumtangaza Kristo, hakika ungebarikiwa kwa hiyo kazi nzuri. Roho Mtakatifu akushuhudie na kubadilisha hii site iwe ya manufaa kwa watu wote waliookoka au ambao hawajokoka, ili wasiookoka wasipotoke na kuto mwamini Kristo.
Munishi posted 3/6/07 10:19 AM    
EDNA ASANTE KJWA MAONI YAKO.Unathibitisha kwamba hao unaowaita watumishi wa Mungu huenda wakatubu wakaingia mbinguni.Hilo ndio lengo la web site hii. Hatutaki tuwakose mbinguni, ndio maana tunayakemea maovu katika huduma zao. Kama kwa kufanya hivyo kutanikosesha mbingu, hiyo sina hakika. Labda wengine wanisaidie hapo. Kuhusu watu kuokoka, hiyo ni kazi ya mwokozi. Siamini kwamba kuwavuta watu kwa Yesu ni kufichiana dhambi. Wa kuokoka ataokoka akijua huku mambo yote ni uwazi. Yanayosemwa uvunguni yanawekwa peupe. Yanayotendwa kwa siri yanafichuliwa. Huo ndio upendo wa kweli. Kuonyana na kushauriana kadiri tuonavyo kuwa siku ile inakaribia. Yesu anakuja kuchukua kanisa lisilo na mawaa. Tukiogopa kuwakemea watu kama kina kulola na wengine wa jinsi yao basi maana nzima ya wokovu itakuwa imepotoshwa. Sisi sote ni wanafunzi wa Yesu. Tatizo ni pale watu wanapojipachika madaraka ya kiroho wasiyokuwa nayo. Wanajiita majina makubwa wakifikiri yataongeza chochote kwenye huduma zao. Hebu tizama kila mtu siku hizi anakazana kujiita DR, MTUME, NK. Je hiyo itamfanya aache kuwa mwinjilisti huduma ambayo ndiyo aliyoanza nayo? Nani aliwadanganya kwamba wakiwa na taito hizo ndipo huduma zao zinapokuwa bora zaidi? Hayo ndiyo mambo ambayo lazima yakemewe. Mimi ninamwamini Yesu anitosha. Simuamini KULOLA WALA KAKOBE. Yesu amenipa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu inanitosha. Sasa naweza kupeleka haja zangu kwa Mungu bila kupitia Kulola.Mnamuogopa kwa sababu amewanyanganya uwezo wa kumwendea Mungu. Lazima muombewe badala ya kuomba, Tena lazima musomewe neno la Mungu badala mujisomee wenyewe. Uvivu wenu kiroho ndio unaowafanya muwaone kina kulola ni watu wasiowezakemewa wanapokosea. Mnakosea. Hakuna mbingu ya wenye dhambi wanafiki. Na kama ipo, sitaki kwenda mbingu hiyo.
Edna posted 3/6/07 12:31 AM    
Sawa Ndugu Munishi nimekuelewa vizuri, na kama unaona uko sahihi kukosoa maovu yao ili watubu, ina maana una uhakika asilimia 100% kuwa hayo uyasemayo ndiyo wayafanyayo.Na uhakika huo uwe si wakusimuliwa au kusikia kwa watu, bali uwe umeshuhudia wewe mwenyewe binafsi kama Munishi. Na kitu kingine mimi najua ya kuwa biblia ni jibu la mambo yote, nikimaanisha kuwa ukimwambia mtu okoka bila kumpa maandiko atashangaa kuokoka maana yake nini anakuwa haelewi, ila ukimpa maandiko ni rahisi kugeuka katika njia zake mbaya na kumgeukia Bwana Yesu.Nikimaanisha ya kuwa unapowakosoa hawa watumishi ni vizuri kama ungeweka na maandiko katika mada zako, ambayo yatawaonyesha kuwa wako kinyume hata na neno la Mungu, na ambayo yatawafanya watu wengi wasikuone kuwa wewe unahukumu bali wajue kuwa uko sahihi.,na hata wao walengwa wakiona watasema kumbe!"Kweli yatupasa kutubu.kwa sababu neno ndivyo lisemavyo. Huo ni ushauri wangu tu na maoni yangu. Napia napinga unavyosema kuwa """""""Mnamuogopa kwa sababu amewanyanganya uwezo wa kumwendea Mungu. Lazima muombewe badala ya kuomba, Tena lazima musomewe neno la Mungu badala mujisomee wenyewe"""""""". Inawezekanaje mtu kunyanganya watu uwezo wa kumwendea Mungu, mtu ambaye ameokoka na kumjua kristo, sawa ndiyo kuna kuombewa ila Wokovu ni wa mtu binafsi, kumwendea Mungu na kumweleza haja zake kwani Mungu wetu ni mwaminifu. Na kwa mtu aliyesimama na Yesu na kumjua vizuri ni lazima kusoma neno na kulielewa kibinafsi si kutegemea watumishi wa Mungu mpaka wakusomee, mbona mtu wa namna hii hufa kiroho na ataijuaje kweli kwa kutosoma neno la Mungu? Na si kwamba hao watu hawapo makanisani ndiyo wapo, ila si kila anaye comment kusema kuwa unawahukumu watumishi wa Mungu yuko kama unavyofikiria, IlA SIDHANI KAMA UNGEKUWA UKIANDIKA MADA UNAWEKA NA MAANDIKO KAMA KUNA MTU ATAKAA NA KUPINGA MADA HIYO, KWANI ATAKUWA AKILIPINGA NENO LA MUNGU. Ni hayo tu ndugu Munishi. Be blessed
jangala posted 3/7/07 7:04 AM    
Jamani mpooo!! Hapa naona mada imepamba moto. Mimi sijaokoka, ila ni mkatoliki. Nimekuwa nikiwapinga wanaojiita WALOKOLE kwani wengi wao hawatendi yale wayasemayo. Mi huona kama WALOKOLE wote ni matapeli. Wanahubiri kwenye TV, na wanatumia kamera kusababisha kile wanachokiita miujiza. Lengo lao linakuwa ni pesa kuliko kuhubiri injili. Japo sisi wakatoliki hatujigambi kuokoka, lakini tunafanya mengi ya kuisaidia jamii. Hatujisifu lakini mtu kama mama teresa anasifiwa duniani kwa kazi nzuri ya kuwajali masikini. Lakini kama Munishi anavyowakemea wahubiri matapeli wanaopenda vitu kuliko utumishi,mimi nakubaliana na Munishi. Kwangu napata picha kwamba siyo WALOKOLE wote ni matapeli. Ikiwa siku moja nitaamua kuokoka natamani kuokoka kweli na siyo kucheza na Mungu
Luka posted 3/7/07 4:18 PM    
Tafadhali sana Munishi ninakuomba ufanye maombi ya kufunga. Ninaandika kama nilivyokuandikia mwanzo, fanya maombi ya kufunga ili Bwana akuondelee hiyo roho ya error. Bwana Yesu atakonyesha ulipopungukiwa. Ahsante sana.
Munishi posted 3/8/07 9:07 AM    
Nimeitikia wito wako. Nilipofunga na kuomba, ndipo nilipoonyeshwa jinsi shetani anavyowaingia hao mnaowaita watumishi wa Mungu na kuwajaza roho ya kiburi. Wameharibu Kazi ya Mungu duniani na Mungu amechukizwa nao. Hawatanyanganywa huduma lakini Bwana hayuko pamoja nao. Ndio maana wamebaki kutunga miujiza ili watu wawaone kwamba bado wako. Wanafanya kimwili siyo kiroho. Wanapenda pesa kuliko Mungu. Zote hizo ni dalili za siku za mwisho. Wanatamani kuabudiwa kama Mungu ndio maana wamejiongezea ulinzi. Mbaya zaidi wanalindwa na silaha za moto. Ni rahisi kumuona Bush wa marekani kuliko kumuona Kulola na Kakobe. Ni wakuu kuliko Yesu mwenyewe ambaye alimwambia Zakayo ashuke mkuyuni. Maisha yao hayana tofauti na wauza madawa ya kulevya kwani wanavyolindwa utadhani wanatafutwa na polisi kwa makosa ya jinai. Lakini hivi karibuni itaundwa tume ya kuwachunguza hawa matapeli wa kidini. Ni wabaya kuliko majambazi kwani wanakuibia kila siku. Majambazi huwaibia watu mara moja kesho wanaenda kwa mwingine. Lakini hawa wanaojiita watumishi wa Mungu, wanakuibia mpaka ubongo wako wa kufikiri. Wanakutajia Mungu wakijua wazi huwezi kubishana na Mungu. Lakini sasa ikibidi watu lazima wajifunze kuhoji hata malaika wacha Kulola. Biblia inatuasa kuzijaribu kila roho kuona kama zinatokana na Mungu. Nasikitika kusema yale niyaonayo kwa hawa mnaowaita wapakwa mafuta, yanaashiria kwamba wanamtumikia shetani huku wakijivika mavazi ya kondoo. Ndio maana injili imewaishia sasa imebaki kujibandika majina. Utasikia Mtu anajiita DR. na wakati madarasa yake ni ya chini. Kama anaweza kudanganya kuhusu elimu yake, nini ambacho hawezi kudanganya? Ni kweli kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa na hekima. Kwa nini wasitosheke na hekima waliyoipata kwa kumcha Mungu? Mbona wanakazana kujiaminisha kwa watu wakitumia majina kama MITUME, DR, FOUNDER, NABII WA MWISHO, POWER MIRACLE BABY PASTOR, NK? Mungu atusaidie tuwajue hawa wezi wanaotuibia wakitumia silaha ya biblia. Neno la Mungu ni silaha kali ambayo ikitumiwa vibaya hakuna serikali duniani inayoweza kuzuia madhara yake. Mitume wa uongo walipoamua kwamba washirika wao wanywe sumu ili wawahi mbinguni, Serikali ya Amerika haikuweza kuzuia hilo. Tanzania msipojihadhari mapema, Siku moja Kulola anaweza kuamka vibaya aone kwamba uzee wake unampeleka pabaya, aamue kwamba sasa inatosha wafuasi wake wote wauze kila kitu na waende Mwanza mlimani kumngoja Yesu hapo. Msishangae kuwaona hata wabunge wakielekea Mwanza kumngoja Yesu huko. Ndivyo yalivyo madhara ya imani potovu. Mungu ameweka askari wake kuhakikisha hilo halitendeki. Na kama litatendeka watakaotapeliwa watajilaumu wenyewe kwani wameonywa tayari.
Luka posted 3/9/07 5:43 PM    
Ndugu Munishi ninasikitika kukwambia kwamba umepotea sana . Yaani inatisha sana kusoma hayo unayoyaandika. Ume-backslide bila wewe kujua. Ni huzuni sana kuona mtu kama wewe umefungwa na adui kiasi hiki. Inabidi wakristo wengine tufunge na kuomba kwa ajili yako Munishi. Shetani amekufunga minyororo bila wewe kujua. Pole sana Munishi. Kwa kweli mimi nitakuombea sana. Yaani umeuacha kabisa upendo wako wa kwanza. Yesu anarudi tafadhali sana tubu. Ahsante sana. bye
Munishi posted 3/10/07 10:07 AM    
Endelea kuniombea niwe na ujasiri wa kuwakemea matapeli waliojiingiza kwa siri kanisani. Siku za mwisho lazima Mungu alisafishe kanisa lake. Liwe safi tayari kungoja kunyakuliwa.
MSHIRIKA EAGT posted 3/12/07 8:06 AM    
Ndugu Munishi Bwana Yesu asifiwe. Mimi ni mshirika wa EAGT kanisa analoliongoza Kulola. Nimesoma mengi hapa yanayomhusu Kulola. Kwanza nampongeza Askofu Kulola kwa kazi yake nzuri ya kuhubiri injili. Ushuhuda wake unaeleza jinsi alivyopata mateso siku za mwanzo akitembea kwa miguu kuihubiri injili. Je wanaomsakama hapa wanataka aendelee kutembea kwa miguu katika uzee wake? Binafsi sitopenda hivyo. Lazima kuwe na mabadiliko katika kazi ya injili. Na kama itabidi mchungaji awe na kagari au pikipiki na baiskeli sioni ubaya wowote hapo. Kile ambacho nakubaliana na Munishi ni pale kanisa linapogeuzwa kuwa kampuni ya mtu binafsi. Hapo sikubaliani. Kweli kanisa linapaswa kuwa mali ya Yesu na waumini wote tunatakiwa kufaidika na baraka za Mungu angaa kwa kiwango kidogo. Kama nilivyosema nakubaliana na Askofu kupata gari, nyumba na pia kuvaa vizuri. Lakini hali hiyo isimpate askofu pekee na huku washirika hali zetu zikiendelea kuwa duni. Mbaya zaidi kama uduni huo wa maisha utasababishwa na michango isiyoisha kanisani. Nimekuwa mshirika kwa miaka zaidi ya ishirini, na kile nilichokiona hakinipendezi. EAGT imegeuka kuwa mali ya mtu mmoja. Mwaka unapoanza tuanaanza michango ya mikutano ya nje ya mzee Kulola. Kila mshirika lazima atoe kiwango fulani cha pesa kuufanikisha mkutano huo. Siku ya mkutano ikifika, kama kawaida Askofu atafika na kuanza mahubiri ya siku kumi au zikipungua siku saba. Kila siku lazima tutoe sadaka. Siku mbili za mwisho wa mikutano, kampeni kali hupita kutuhamasisha tutoe zaidi kwa ajili ya mtumishi wa Mungu. Mchungaji mwenyeji wa mkutano hutuomba wale tunaoweza kununua zawadi maalum kwa ajili ya Askofu na mke wake. Kweli tunajitahidi kufanya hivyo na kila mwaka mambo yanakuwa hivyo hivyo. Kinachonisumbua ni jinsi gani injili inakosa kupewa kipaumbele na michango na matoleo inapewa umuhimu zaidi. Katika kanisa letu kuna utamaduni wa mwinjilisti kubeba sadaka yote inayokusanywa siku zote za mkutano wa nje. Hilo ndilo linalonikera. Mkutano tulichangishwa kuufanikisha, halafu ukifanyika Kulola anabeba sadaka zote, kisha na zawadi za hiari juu yake. Mchungaji aliyeandaa mkutano anabaki na madeni, washirika tunabaki tumekauka mifukoni kiasi kwamba hatuwezi hata kumudu chakula majumbani mwetu. Wale wanaosemekana kwamba wameokoka kanisa linakuwa hata halina pesa za kuwafuatilia ili wadumu katika imani mpya ya wokovu. Na kwasababu kanisa ni masikini halina hata vyombo vya kuhubiria, wale wageni waliookoka wakiona mbwembwe za Kulola hazipo kanisani, wanarudi kule walikokuwa. Tunabaki kama tulivyokuwa, tukingoja mwakani tuanze michango ya mkutano mwingine. Ukweli ni kwamba hali hii inatufanya washirika mafukara na wengi hukata tamaa ya kuendelea na imani. Wachache tunaobakia hali zetu zinazidi kuwa mbaya. Hii inanipa kujiuliza Mungu ni wa kuwabariki wachungaji pekee na siyo washirika? Kwa mtindo huu hakuna mshirika wa EAGT atayeondokana na uduni wa maisha. Askofu anatuhimiza kuvumilia magumu ya imani huku yeye akijitajirisha na pesa zitokanazo na sadaka. Pengine ndiyo maana Askofu wetu haendi sana vijijini wanakohitaji kweli injili, na kama atapitia huko, mkutano utakuwa wa siku moja. Lakini kwenye ile miji yenye wazito, mkutano utaunguruma siku kumi. Je huku siyo kupenda pesa japo Kulola husema hazipendi? Lini makanisa yatakua kiasi cha kuwajali washirika wake ikiwa kila mwaka tunachangishwa kufanya mikutano ambayo lengo lake ni kuchangisha pesa kuliko kuhubiri? Pengine kuna wengine ambao hawakufurahia mada hii kuanzishwa hapa, lakini binafsi ninaona umuhimu wake. Kwa miaka ishirini nimeona watu waliokuwa na mali kiasi wakiingia EAGT na baada ya miaka mitatu tu unaona hali zao zinakuwa duni kiasi kwamba Askofu aliyekuwa akiwatembelea kila mwaka, anaacha kufanya hivyo. Je EAGT ni kanaisa la kuwafilisi waliokuwa navyo na kuwaacha na kwenda kuwafilisi wengine? Mbona isiwe kwamba kanisa ni mahali pa washirika kujifunza mbinu mpya za kujikimu kimaisha? Je kwa Mtindo huu tutafika?? Nampongeza mtumishi wa Mungu Munishi kwa kuliona hilo. Badala ya kumsakama Munishi ningewaomba wote walioumizwa na michango ya kila siku kila mwezi na kila mwaka EAGT tusema basi. Imetosha.
MUNISHI posted 3/12/07 8:35 AM    
Kweli Mungu ni mwema. Anatupenda sote.Nashukuru ukweli unaanza kufichuka. Wengine walidhani nina chuki binafsi na Mwinjilisti Kulola. HAPANA. Yanayoniumiza moyo ni hayo mliyosikia kutoka kwa mshirika wa EAGT.Ni kweli EAGT Tanzania nzima hufanya michango kwa ajili ya mikutano ya Kulola. Binafsi nimewahi kusafiri mikoani na Askofu Kulola na hali iko hivyo. Wachungaji wa mikoani hali zao ni duni, huku wanachangishwa pesa kila mwaka. Maoni yangu waachwe nao wakuze makanisa yao ili wawasaidie wenye mahitaji katika mashina yao. Kuweka bomba ya kunyonya pesa zote zimuelekee kulola siyo sawa. Kulola mwenyewe alitoka TAG ili awe huru kuihubiri injili ambayo sasa hataki wengine wawe huru kuihubiri bila kamba za EAGT. Pole sana ndugu yangu unayesema kwamba kanisa limekuwa sababu ya kufilisika kwako. Sitaki nikuahidi baraka za mazingaumbwe, lakini nitakuambia kwa ujasiri wote kwamba siyo mapenzi ya Mungu uwe hivyo Kulola alivyokufanya uwe. Omba Mungu akuambie hatua gani uchukue.
MPITA NJIA posted 3/12/07 5:12 PM    
Jamani huyu mzee KULOLA yuko wapi? Au ndiye anayejiita EDNA? Hajasikia lawama zote hizi kumhusu. Si aje hapa aseme YOOOOOOOOO wanangu mimi sitaki pesa. halafu mkutano ukiisha pesa zote zipelekwe chumbani kwake akahesabu yeye na mkewe na Dani mtoto wake. Jitetee mzee. Hapa maji yamezidi unga. Acha kuwatuma kina EDNA. Kauli yako ndiyo itakayowafanya washirika wa EAGT watulie. Safari hii wanaonekana wameamka usingizini. Wanaelekea kuijua kweli iwaweke huru. Uhuru wao utategemea na kweli wanayoijua. Na hapa inaonekana wanaambiwa kweli. Usishangae kwenye mikutano yako wakaja wasukuma wachache pamoja na familia yako. Watu wamejua kwamba Temeke siku kumi za mkutano ni ujanja wako uvune pesa nyingi na siyo kuvuna watu wengi kwa Yesu. Mbona kanisa la TEMEKE miaka yote liko lilivyokuwa? mikutano yako Temeke maana yake nini kama washirika hawaongezeki. Jengo ni lile lile. Mchungaji MASALU hoi vile vile. Pesa zote unabeba wewe na kudai umemwachia kondoo ambazo hurudi zizini mwao mara tu unapopanda ndege kwenda mwanza. Ndiyo maana watu kama MABOYA walipojaribu kuinuka wawe wahubiri kwenye EAGT uliwagonga nyundo utosini ubaki wewe na DANI mwanao. Kweli Tanzania nzima huna watoto wa kiroho ila mwanao Dani? Afurahie ukiwa hai. Ukiondoka hakuna atakaembeba DANI. Unamharibia humtengenezei. Mwache asimame kwa miguu yake mwenyewe. utambeba hadi lini? Mungu hapendi ufanyavyo. Ni wasi wasi wako tu. Kama ukiamua kuwainua wanao kiroho bila kujali kama ni WASUKUMA au wanao wa kuwazaa kimwili, sasa hivi wala usingekuwa unahangaika kuandaa mikutano ya lengo la kutafuta pesa. Miaka yako kwenye huduma siyo ya kujifungia chumbani na mkeo kuhesabu sadaka. Kiwango hicho ulitakiwa uwe umepita zamani. Ona ulivyowafanya kina Mwasota na Mwasumbi. Uteseke nao mwanzoni, uwatupe uzeeni. Heshima ya mzee kama wewe ni nini kama siyo kina Mwasota na Mwasumbi kuwa karibu nawe uzeeni? Itaeleweka ni huduma kwani hawa ni WANYAKYUSA nawe ni MSUKUMA. Kwani lazima huduma yako isukumwe na WASUKUMA peke yao????
John posted 3/20/07 7:11 PM    
Habari zenu wachangia hoja na mtoa mada! Nadhani yamesemwa mengi kuhusu huyo Kulola na wengineo waliotajwa kwa majina na wasiotajwa. Cha msingi hapa hatujengi ufalme wa Mungu kwa malumbano haya ya hoja, Hii inaonesha ni kwa kiasi gain tumepungukiwa na maongozi ya Roho Mt. Kwa mtazamo wangu na uzoefu wangu ndani ya hilo kanisa linaloitwa la Mzee Kulola kama kweli ni kanisa lake, japo siamini kama ndivyo kibiblia kwani sijawahi kuta kibao kimeandikwa KULOLA CHURCH. Kuhusu suala la kuoa na kuoana ni hiari ya mtu ndani ya kanisa hilo! Mambo ya kuchaguliwa mke au mume kama huyo Mzee alikushauri, ushauri una hiari ya kuukataa au kukubali na ndio maana unaitwa USHAURI, kama ulienda kichwakichwa ukakubali pasipo kuchuja katika ulimwengu wa roho hapo kosa ni lako sio la mzee wa watu. Ni wangapi ambao baba zenu waliwashauri wake wa kuoa, je niulize ni wote mlioshauriwa mlikubali kuoa hao wake au waume? Hebu tutumie akili tu za kawada hapa, hivi huyo Kulola atawatafutia vijana wangapi wake na waume? Karibu kila wiki kuna ndoa nyingi zinafungwa ndani ya EAGT, je hao wote wameunganishiwa mambo yao na huyo Mzee? Nachelea kusema kwamba hii dhana si ya kweli.Suala la ndugu anayejiita mshirika wa EAG(T) kuhusu michango, nadhani nao ni ukosefu na upungufu wa kukua kiroho. Kutoa ni moyo usambe si utajiri. Kama kulingana na ulivyosoma neno na unaona kwamba ukitoa kwa ajili ya mkutano utabarikiwa toa, huoni baraka ndani yake, achana nao. Sijawahi sikia mchungaji yeyote akilazimisha washirika kutoa kwa ajili ya mikutano ya Kulola, bali hupigwa panda kwamba mwenye nacho atoe kwa ajili mkutano. Kama yuko Mchungaji aliyelazimisha washirika wake kutoa basi huyo ni tatizo lake binafsi na sio la Mzee wa watu - Kulola! Ni omba omba wangapi wako barabarani ambao hujawapa kitu, wajane wangapi wamebisha hodi kwako, je biblia inasema nini kuhusu hao wahitaji?? Pia hiyo michango watu watoayo kwa ajili ya injili kwenye mikutano ya Mzee Kulola na si hiyo tu hata na ya watumishi wengine Munishi nawe na wengine wakiwemo huwa si ya Mtu mmoja tu! Kuna watumishi wa aina tofauti tofauti ambao hufaidika nayo na nadhani ni halali yao kibiblia. Nimeshuhudia suala la michango ya injili hapa Ulaya karibu kila mwezi, tena sio kama kwetu, huku waweza pewa “bill” kabisa yenye account number ya kanisa uende uka-deposit hela benk, wengine hadi kwenye websites zao bado wanaomba michango miaka nenda rudi, je hawa nao ni wezi wanaosababisha umaskini kwa wazungu wenzao? Cha ajabu ni kwamba ndio wanaobarikiwa sana kuliko hata sie waafrika. Unashindwa kubarikiwa kwa sababu ya roho ya korosho, unatoa huku ukiwa na manung’uniko kibao. Nakushauri acha kutoa nenda kanunue mchicha ule na jamaa zako walao mshibe kuliko kujitafutia mateso ya kinyongo na wachungaji wa watu. Calling the old “cult leader” kwa sababu ya kuwaomba watu michango is a blasphemy!!!! Na nadhani aliyesema hivyo sio mtu wa Mungu wala mkenya kama asemavyo bali kajificha ndani ya utaifa huo na pia hamjui Mungu. Na hapo ndipo ninapoanza kuhisi kuwa hii mada imeingiliwa na majambazi wa imani. Hata kama unayo imani kubwa na kujihisi kuwa uko juu kiroho kuliko wenzako, si vizuri kutumia lugha kama hizo. Mwisho, niwaombe kuisimamia na kuishindania imani ambayo tumekabidhiwa na Bwana mara moja, naam na tuangalie pia miongoni mwetu mtu asije akaipungukia imani ni hatari kwa kipindi tulicho nacho cha Roho Mt. kuliandaa kanisa. Tuache kusemana japo ni kweli tuna uhuru wa kujieleza na kutoa maoni lakini tukumbuke kuwa “hakuna uhuru ulio huru”. Hii column ya Mh. Munishi nadhani itumike kujenga zaidi kuliko kusababisha mioto isiyo na sababu ndani ya watu, pia wachangiaji na wawe wakweli kwa kutoa na kueleza yale waliyo na ushahidi nayo sio wayasikayo kwa watu.Mbarikwe na Bwana wote wenye mapenzi mema na kazi ya Mungu pamoja na kuwaombea watumishi wake!
Abel A. Kinyondo posted 3/20/07 7:51 PM     Click here to send email to Abel A. Kinyondo  
Kulola na Lazaro walishasameheana na yote yameisha. KWa wewe kuongea uliyoongea unahitaji msaada wa Mungu. Mungu akusaidie maana kwakweli kazi ya Mungu uliitenda kwa nguvu. Nafikiri ikaliko nafasi!!!
Kijenge posted 3/23/07 5:21 PM    
Jamani hamjambo? Kwa wale waliookoka BWANA YESU ASIFIWE SAAANA. Mi natoka Kijenge Arusha. Naona watu hapa hawatumii majina yao kamili, pengine Munishi, nayo pia huwezi kuwa na hakika kama ni yeye. Lakini kwa sababu yeye ndiye mhariri wa mtandao huu, wacha niamini ni yeye. Mimi nitaajiita Kijenge mtaa ninaoishi. Nimesikia mengi hapa, na mniruhusu nikubaliane na wale wote wanaolalamika kuwahusu wahubiri matapeli. Ni ukweli kwamba wapo wezi wanaowaibia watu wakitumia neno la Mungu. Wasiposemwa hawatajua kama wamegundulika. Mfano hapa Arusha amezuka jamaa mmoja anayejiita GEORDAVIE KASAMBALE. Huyu bwana amekuja na ngurumo ya upako. Hiyo ndiyo kauli mbiu yake. Tayari ameanza kuwatapeli wakristo Arusha. Wote wanamiminika kwake wakidai kuifuata miujiza. Nijuavyo mimi ni kwamba miujiza itawafuata waaminio na siyo waaminio kuifuata miujiza. Nakubaliana na msemaji wa awali aliyesema uvivu wetu kuomba umetugeuza kuwa waombewaji. Tena msemaji huyo aliongeza kusema kwamba uvivu wetu kusoma neno umetufanya tusomewe na kisha tutafsiriwe vibaya. Tukisema tunyamaze, watazuka wengi wa kututapeli. Kama huyu wa Arusha mtakuja niambia maana yeye hudiriki hata kujiita Yesu mwenyewe. Nyumbani kwake kuna bendera ambayo pia iko kanisani. Kwake kunaitwa mji wa DAUDI. Kumuona siyo rahiri analindwa kuliko Bush wa Marekani. Dalili moja ya kuwajua hawa matapeli wa kiroho ni jinsi wanavyolindwa. Hawataki waliowaibia waje kudai pesa zao. Kama kweli ni watumishi wa Mungu mbona wanalindwa na bunduki? Yesu alimkemea Petro alipojaribu kumlinda akitumia upanga. Alimwambia kama angetaka, angeagiza jeshi la malaika waje wamlinde. Mwana wa Mungu ambaye alikuwa Mungu alijifanya mtu ili awapate watu. Hawa matapeli ambao roho ya tamaa ndio iliyowajaa, wanajifanya siyo watu wa kawaida, na sijui watawapata kina nani. Lakini wako wengi wanaotaka utajiri wa haraka kwa njia za mkato.Ndio hao wanaokimbiza pesa kwa hawa matapeli ili ziombewe ziongezeke mara dufu. Watu kama hao siwahurumii kwani tamaa yao ndiyo inayowafanya wawakumbatie wahubiri matapeli. Nawaomba tuwasaidie wale wachanga wasiojua kupambanua. Wajiadhari na matapeli kama kina JOERDAVIE na wengine wenye roho za udanganyifu. Mungu atusaidie sana nyakati hizi za mwisho.Kwako msemaji wa hapo juu. Yaani unadhibitisha kwamba Kanisa la Kulola linawachangisha watu pesa isivyo halali, na kwa hiari wakitoa wajilaumu na wasimlaumu Kulola? Kwangu naona wa kulaumiwa ni hawa wahubiri matapeli kwani hutumia kila mbinu ili kuhakikisha kwamba wamewatisha washirika wao ili watoe kama kumtolea Mungu kumbe wanawatolea wao.
FRIDA posted 3/31/07 5:15 PM    
Shalom!!Napenda kuongelea kuhusu NABII Geordavie aliyesemwa na mtu wa Kijenge.Naomba nichangie maada hiyo!!Yesu aliposema watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa hakukosea. Mungu ameleta Nuru duniani lakini watu wamependa giza kuliko nuru yenyewe. Tena nawaambia kabisaaaaaa! muelewe mtu huyo sio Tapeli wala sio Nabii wa uongo ni mtu aliyetumwa na Mungu mwenyewe.Wenye masikio na wasikie pia wenye upako, maono na mafunuo wamwulize Mungu wao.Acheni kusikiliza maneno ya Wachawi na wapenda dini wanaojaribu kuzusha uongo ili watu wasifunguliwe wala wasipate miujiza yao. Unafikiri wasipojaribu kuzusha uongo watakula wapi???Someni basi angalao maandiko mpate ufunuo? Na kama nyie ni watu wa Mungu tunayemwabudu aliyemtuma mwanaye Yesu ili aje duniani kutukomboa mwulize basi Mungu, mtu huyu ni wewe umemtuma ama la??Sio mnakurupuka na kuanza kusema anatenda miujiza mno lazima katoka kwa shetani. Mnaamini nguvu za Giza kuliko nguvu za Mungu kwa kuwa zamani mlikuwa mmefanya makao huko kwa waganga wa Kienyeji.Anawezaje mtu kutumika kwa jinsi hiyo, someni basi hata maandiko?? MATAYO MTAKATIFU 12: 24-31.Nasema huyo mtu anayedai ni Kijenge, aliyemsema Mhe. Nabii Geordavie asipoomba msamaha lazima Mungu atasimama. Sasa kazi kwake kukanusha usemi wake au kusubiri malipo ya kumnyoshea Mtumishi wa Mungu kidole.Mwulizeni Mungu awapatie ukweli kuhusu mtu huyu kama mnawasiwasi naye. Mliomba mpaka mapovu yakawatoka eti huduma ife sasa mbona????Ina maana Mungu wenu ni kiziwi basi? Kama mnamwabudu Mungu wa kweli na Geordavie ni wa uongo mwambieni Mungu wenu amwangamize kwani watu wengi wanamfuata na miaka miwili ijayo makanisani watabaki wachungaji na wake zao. Maake hata watoto nao watafunguka na kujua ukweli watakwenda kwa Geordavie sasa kazi kwenu.Heri mtu yule asiyekuwa na mashaka na mtu huyu. Kwani anafungua watu kwenye vifungo mbali mbali. Nendeni mkajionee mambo makubwa Mungu anayoyafanya kupitia mtu huyu.Basi mbarikiwe na Mungu awape macho ya rohoni mpate kujua jema na baya.Frida.
Kithuku posted 4/10/07 1:05 PM     Click here to send email to Kithuku  
Toba, tumekwisha! Huyo mnayemtaja si yule NGURUMO WA UPAKO ambaye radio za FM za Arusha zilitangaza kwamba aligeuka joka kanisani kwake? Na mama mmoja aliyemwona akigeuka nyoka akatishiwa kwamba ole wake aseme, akijaribu tu atakufa! Na kweli alipomsimulia mumewe kile kisa alianguka chini na kufa palepale. Mumewe alipeleka malalamiko polisi lakini kutokana na kukosa ushahidi, suala halikufikishwa mahakamani. Lakini tukio hilo limezungumzwa sana Arusha mwaka jana, na taarifa polisi zipo. Ngurumo mwenyewe alipoulizwa alikana kumfahamu mwanamke huyo. Sasa huyu ndiye mnayemsifia ati ni nabii? Nabii wa kitu gani? Hebu acheni masikhara!
KIJENGE posted 4/20/07 2:03 PM    
JOE DAVIE ni Tapeli kama wale wengine.Wanaomfuata ni wale wasojua watokako wala waendako.Mi sijali kama aligeuka nyoka wala shetani. Hata akija kama malaika wa nuru na awe anapotosha injili nitamkemea. Nimefurahi sana kwamba mada ya kuwajadili matapeli wa kidini imeanzishwa hapa. Kulola na KAKOBE, JOEDAVIE na MWAKASENGE, wote mnatakiwa kujihadhari na matapeli kama hawa.
Deus posted 5/2/07 10:31 AM    
Munishi, Wewe huna tofauti yoyote na wale heresy hunters ambao kazi yao hudhani kuwasaidia watu na kumbe la! ni kwamba wanatumiwa na adui ibilisi kuujenga ufalme wake. Kwa undani kiasi mimi ninakufahamu wewe pia na ni mangapi maovu uliyoyatenda ukiwa kama mkristo unayedai umejazwa na Roho Mtakatifu? Usitake tuyaweke bayana maovu yako.Hata hivyo watu wengi wamekushauri vizuri na ni vema ukasikiliza ushauri wao. Hiyo kazi unayoifanya siyo ya Mungu bali upo upande wa adui ambaye ni shetani. Mungu akusaidie uligundue hilo na utubu na kukaa sawa maisha yako ya kiroho
Deus posted 5/2/07 10:34 AM    
Munishi, Wewe huna tofauti yoyote na wale heresy hunters ambao kazi yao hudhani kuwasaidia watu na kumbe la! ni kwamba wanatumiwa na adui ibilisi kuujenga ufalme wake. Kwa undani kiasi mimi ninakufahamu wewe pia na ni mangapi maovu uliyoyatenda ukiwa kama mkristo unayedai umejazwa na Roho Mtakatifu? Usitake tuyaweke bayana maovu yako.Hata hivyo watu wengi wamekushauri vizuri na ni vema ukasikiliza ushauri wao. Hiyo kazi unayoifanya siyo ya Mungu bali upo upande wa adui ambaye ni shetani. Mungu akusaidie uligundue hilo na utubu na kukaa sawa maisha yako ya kiroho
Return To Message Board

http://munishi.com  | Post New Topic