Return To Message Board
Author Topic:   NGURUMO YA UPAKO
PIUS posted 11/5/07 12:30 AM    
Tumsifu Yesu Kristo1
Kwa kweli imefika wakati ndugu zangu ktk Kristo tuache Kuwanyooshea vidole watu bila kujali anafanya kitu gani, kwani Mungu aliumba watu wazuri lakini Ibilisi akaweka sumu yake ndani ya watu wa Mungu. Hivyo mimi sishangai kuona watu wanatumikishwa au wamefungwa katika ulimwengu wa roho. Huyu anaye itwa Geor Davie pia naye ni mtu wa Mungu kama watu wengine sasa anachokifanya yeye na anapata wapi Nguvu anazo tumia hilo si juu yangu ila pale wewe uliyeekoka kama unakosa amani kwenda kwenye huduma yake usiende, kama umesikia kuomba kwa ajili ya huduma hiyo omba kwani ni watu wengi sana wanaohudumiwa kule ambao ni ndugu katika Kristo. Eti kusema kuwa Mungu basi na amuadhibu kwa sababu anafanya kwa Nguvu za giza hicho ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa, kwani sivyo Mungu anavyo fanya kazi, ingelikuwa ndivyo basi Shetani siku ya leo angekuwa tayari amekwisha pokea hukumu yake. Ebu wewe uliyeeokoka jingalie maisha yako yamekuwa ya kumpendeza Mungu kiasi gani hata unakuwa tayari kuhukumu? Ebu wape taarifa watu wa Mungu tarifa ya kile ulichokiona wewe ktik maono yako kwa njia ya Ulimwengu wa roho pia, ninamaanisha Umbe watu waweze kuijua ile kweli. Jamani pia Mjue Shetani ananafasi kumbwa ya kutenda hapa Duniani kumbuka jinsi ile alivyo mchukua Yesu Kristo hadi kileleni na Kumuonyesha fahari zote za Duniani. Pia Siku ya leo bado shetani amekuwa akiwatumikisha watu wengi wa Mungu bila wao kujijua. Nataka kukuambia kuwa kuna Huduma nyingi amabazo zilianza kwa uwepo wa Mungu lakini sababu ya watumishi katika huduma hiyo kujisahau wamemuachia Shetani aongoze huduma zao lakini hapa hatuwaoni kwa sababu tulisha jenga imani juu ya kile alichokifanya miaka ya nyuma. Ukweli tunaambia zipimeni hizo roho na imetupasa kuzipima hasa.
Mungu wetu ni Mugu aliye Karibu sana hivyo huitaji kwenda kumtafuta Marekani wala Ngaramtoni. “Mimi ni Mungu niliye Karibu nawe sana na pia mkiijua kweli itawaweka Huru kweli kweli”
MANI YA KRISTO NA ITAWALE MAMUZI NA MAWAZO YENU.
MUNGU AWABARIKI SANA
Wenu katika Kristo Yesu
Pius
Return To Message Board

http://munishi.com  | Post New Topic