|
Author
|
Topic: KUWAKEMEA KULOLA NA KAKOBE JE MUNISHI ANATUMIWA NA SHETANI?
|
DEUS (Moderator)
|
posted 5/5/07 8:25 AM
Munishi, Wewe huna tofauti yoyote na wale heresy hunters ambao kazi yao hudhani kuwasaidia watu na kumbe la! ni kwamba wanatumiwa na adui ibilisi kuujenga ufalme wake. Kwa undani kiasi mimi ninakufahamu wewe pia na ni mangapi maovu uliyoyatenda ukiwa kama mkristo unayedai umejazwa na Roho Mtakatifu? Usitake tuyaweke bayana maovu yako.Hata hivyo watu wengi wamekushauri vizuri na ni vema ukasikiliza ushauri wao. Hiyo kazi unayoifanya siyo ya Mungu bali upo upande wa adui ambaye ni shetani. Mungu akusaidie uligundue hilo na utubu na kukaa sawa maisha yako ya kiroho
|
MUNISHI (Moderator)
|
posted 5/5/07 8:27 AM
Bwana Deus Nimekusikia. Mimi siko upande huo uliosema. Neno la Mungu linatufundisha kuonyana kadiri tuonavyo siku ya kuja kwake inakaribia. Siamini kuwa upande wa Mungu ni kufichiana maovu. Ikiwa kuna yangu unayoyajua siombi uyafiche. Yaseme niyakubali au niyakatae. Yakiwa ya kweli nitatubu ili niwe tayari kumngoja Yesu. Kama nimekuelewa vizuri, una maana ninyamaze ili usiseme yangu. Sinyamazi, wala siwaombi msamaha KULOLA na KAKOBE, Nasimama na niliyosema. Ni kweli ndiyo maana hawakanushi. Kama kusema ukweli ni kumtumikia shetani, mimi sijui. Nijualo ni kwamba Mungu ni kweli tupu na uongo hauko ndani yake. Tena Shetani ni baba wa uongo. Kwa hiyo bwana DEUS ukumbi uko wazi umwage yote unayoyajua kunihusu Munishi.
|
|
KIJENGE
|
posted 5/5/07 12:59 AM
Mzee Munishi wape vidonge vyao. wakimeza wakitema shauri yao. Wamezoea hawa matapeli wanaotumia jina la Mungu kama silaha ya kuwaibia watu pesa. Mimi bado nalia na huyu wa Arusha anayejiita JoeDavie au ngurumo ya upako wa wizi wa pesa za watu. Lazima watu kama hawa wamulikwe. Anajifanya mkuu kuliko Yesu mwenyewe, anajificha aliowatapeli wasimkamate. Analindwa kuliko Kikwete. Sasa tumejua ni kwa nini. Yote wasemayo na ahadi watoazo ni za uongo ndio maana wanalindwa ili wale waliotapeliwa wakirudiwa na fahamu zao, iwe vigumu kuwafikia na kudai mali zao. Lakini hawana bahati. Mzee Munishi ameshatushitua. Tutawaandama kwa mtindo mmoja hadi wakome kuwaibia watui wakitumia neno la Mungu. Ni majambazi hatari kuliko wale wanaotumia bunduki, kwani wakikutisha na Mungu wanaiba mpaka bongo yako unakuwa huwezi fikiri sawa sawa.Ndio maana utawakuta hata wasomi wametapeliwa na hawa jamaa ambao wengi hawana elimu mbali na kutaja jina la Mungu na kutishia watu eti watawalaani wakiyasema maovu yao. Mzee Munishi amesema wa kulaaniwa ni wao. Kwani wanavuna wasipopanda. Hawataki kufanya kazi wanangoja wengine wafanye wawaletee fungu la kumi. Kazi yao ni kuvaa mavazi ya bei ya juu, na kuishi maisha ya kifahari wakati washirika wao hawawezi kumudu mlo mmoja kwa siku. Wanatakiwa kukemewa na watu wanatakiwa kujihadhari nao kama ukoma.
|
|
HABIYE YUSTO
|
posted 7/19/11 2:26 PM
Munishi okoka kwanza acha huo uhuni, pasta kama mnyanyua vyuma? kanisa hilo unalikokota motoni, unahitaji kuchungwa na wewe...............
|