Return To Message Board
Author Topic:   MWANDISHI AWE NA SHAHADA AU KIPAWA?
MWANDISHI posted 4/28/07 8:24 AM    
Je, kigezo cha shahada ya Chuo Kikuu ni muhimu kwa mwandishi? Habari Zinazoshabihiana • Chuo Kikuu Mzumbe na harakati za kudahili wanachuo 4,000 mwakani 02.06.2006 [Soma] • Padri Mosha ajitosa ubunge Vunjo 27.10.2005 [Soma] • Ri-man: Roboti anayeweza kuona, kusikia na kunusa 23.03.2006 [Soma] HIVI karibuni Mtandao wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari (IJNet), ulifanya utafiti kwa kukusanya maoni kutoka sehemu mbalimbali duniani kuangalia kama hoja ya kwamba ni lazima mwandishi wa habari awe na shahada ya Chuo Kikuu katika taaluma hiyo ina msingi au la. Kwa kuwa Tanzania nayo iko katika mchakato kama huo, Mwandishi HASSAN ABBAS ameyakusanya maoni hayo, kila mmoja kwa kuangalia uzito wa mitazamo iliyotolewa. TAALUMA ya uandishi wa habari ni nyeti hasa kutokana na umuhimu wa sekta hiyo ambayo inasaidia kutimiza moja ya haki za binadamu za kusambaza na kupashwa habari habari lakini pia kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa husika. Kwa miaka mingi sasa, kumekuwa na mjadala ambao hapo awali haukuwa rasmi lakini sasa umejitokeza zaidi sehemu mbalimbali duniani; swali kuu likiwa ni je, ni lazima mwandishi awe na shahada ya Chuo Kikuu katika taaluma ya uandishi wa habari, kama ambavyo baadhi ya taaluma nyingine zilivyoweka bayana? Mitazamo imekuwa tofauti tangu zamani. Wapo ambao wanasema kuandika ni kipaji kinachojumusiha uwezo binafsi na uzoefu ambavyo vyote humjengea mtu uwezo wa kuyaona na kuyafafanua mambo kwa hoja thabiti. Katika hili wanaoamini wanasema elimu iwe ya uandishi au taaluma nyingine ni muhimu ili kumsaidia mtu huyo pamoja na kipawa kujua misingi ya kazi hiyo. Kundi lingine ni lile linaloamini kuwa kama ilivyo kwa wanasheria, ili aruhusiwe kuwa wakili na kuweza kutetea kesi mahakamani lazima angalau awe na shahada ya Chuo Kikuu katika taaluma hiyo. Je, mushabaha (mfano) huu unadhibiti inapokuja taaluma ya habari? Wanaoamini katika hoja hiyo wanasisitiza zaidi kwa kuangalia unyeti wa sekta yenyewe na wamekwenda mbali hivi sasa kwa kutaka hata vyombo vya habari visiajiri wale wasio na shahada ya Uandishi. Ni kutokana na uzito wa mada hiyo ndio maana hata taasisi kubwa kama IJNet, ziliamua kufanya tathmini kwa kuwauliza wadau wenyewe wa sekta hiyo kutoka sehemu mbalimbali. Utafiti huo uliofanyika mwezi uliopita, uliibua hoja mbalimbali ambazo mwenyewe ukizosoma kwa mantiki ya nguvu ya hopja si wingi au kuangalkia vipengele vingine, unaweza kupata hitimisho. Hivi ndivyo wadau mbalimbali walivyosema kuhusu mada hiyo:- ========== " Nadhani shahada si muhimu, kwa sababu digrii tu si kigezo kinachojitosheleza. Kazi kwa vitendo na mafunzo kupitia mitaala ya shuleni ni vitu viwili tofauti. Hapa naweza kukutajia majina ya waandishi wengi ambao hawana shahada lakini wanafanya kazi kubwa. =========== " Naamini kujituma ndiko kunakozaa matunda mazuri katika kazi yoyote hasa uandishi wa habari ambao unaangalia zaidi masuala ya uchunguzi. Aakash Santorai. " Kila mara nasikia mjadala kama huu, lakini naamini uandishi unahitaji shahada ili kufanyakazi zake vyema. Waandishi wasipohudhuria mafunzo watashindwa kufanyakazi yao kwa kukosa maarifa. Katika uzoefu wangu nimebaini kuwa watu hutenda makosa kwa sababu ya ujinga. Naamini kuwa kipawa kinakuwa kizuri ukiwa na elimu." Emebet Demeke. " Kuwa mwandishi wa habari shahada ya elimu ya Mawasiliano ya Umma si kitu muhimu sana. Suala hapa ni je, uko tayari kuutafuta ukweli bila woga? Kujituma na kujiamini ndicho kinachokufanya uwe mwandishi mzuri. " Kisha unapopata digrii katika eneo hilo unapata msingi wa jinsi ya kuandika na kumfikia msomaji. Unaweza kuifahamu lugha lakini mafunzo yanakusaidia kujua jinsi ya kuifanya kazi yako tangu mwanzo. Rina Mukherji Machi 23,2007. " Hii ni mada nzuri lazima niseme. Kusema kwamba digrii si muhimu katika fani yetu ni sawa na kusema waliogundua taaluma ya Mawasiliano ya Umma hawana walichokifanya. Hao wanaweza kusema kwamba unaweza kuwa mwanasheria mzuri kwa kukaa kwenye ofisi za wanasheria hata kama hujasoma sheria Chuo Kikuu! " Je, unaweza kuwa daktari mzuri kama hujaenda Chuo Kikuu kusomea udaktari? Kinachotumika katika taaluma hizo nyingine ni lazima pia kiangaliwe katika fani ya uandishi wa habari. Iyke Ogbonnaya Machi 22,2007. " Hii ni mada nzuri. Nafanyakazi katika televisheni nchini Zambia. Sidhani kama shahada ya uandishi ni muhimu sana katika kazi hii. Ingawa taaluma hiyo inaweza kumfanya mtu awe na maarifa na menejimenti nzuri katika sekta ya habari, haiwezi kumpa mtu uhakika kwamba ndio atakuwa mwandishi mzuri. Uandishi ni kujituma. " Kampuni ziendelee kuajiri wafanyakazi ambao hawana digrii..." Sitali Amukena | 22/03/2007
MWANDISHI posted 4/28/07 8:28 AM    
Mimi ni mwanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari na ninafanyakazi katika gazeti la kila siku. Kila mara nimekuwa nikisikia kuwa waandishi wanapaswa kuwa na kitu fulani, nakubali. Lakini elimu ya kiwango cha chini haisaidii, si katika karne hii, karne ya 21. " Kwa sababu hiyo walau diploma ni muhimu. Sisi si tu ni "wahandishi" wa habari bali pia tunapaswa kutafsiri na kupambanua mambo. Milan 22/03/2007 " Hakuna ubishi kwamba kama una uwezo wa kusaka habari unaweza kuwa mwandishi mzuri lakini hii ipo katika masomo karibu yote ya sayansi za jamii, hatujui kwamba unapopata mafunzo inakupa silaha ya kufanyakazi kiufundi zaidi? ============ " Nafahamu hii ni taaluma mpya na nchi nyingi haziwezi kufikia kiwango cha digrii lakini ninachoamini ni kwamba kuwa na shahada katika eneo fulani kunakuongezea uwezo zaidi wa kuifanyakazi hiyo. Nadhani digrii ni muhimu kwa fani zote na iwekwe kama kigezo na kama ikiwa hivyo katika fani nyingine kwa nini isiwe katika uandishi wa habari. Rafia 21/03/2007 ============ " Digrii si muhimu katika uandishi wa habari. Kwa mtazamo wangu uandishi wa habari ni fani inayotegemea sana kujituma kwa mtu. Elimu haimsaidii mtu kuweza kupata habari kubwa au zinazogusa jamii. Kupambana na utendaji wa makosa mbalimbali katika jamii au kuwakabili wala rushwa, hilo ni suala linalokwenda nje ya mafunzo darasani. " Waajiri katika vyombo vya habari wanapaswa kuajiri kwa kuangalia kigezo cha uwezo na kujituma kwa mtu na si rundo la makaratasi mtu aliyoyapata katika safari yake ya masomo. Zaidi ya hapo mwandishi si yule anayekaa kwenye kiti cha kuzunguka akiangalia makosa ya kilugha na kisarufi. Naamini elimu kwa mwandishi iwe ile ambayo imelenga kumjuvya misingi muhimu tu na kumpa ujuzi zaidi na si kuwa kigezo cha ajira. Luke Kapchanga, 21/03/2007
MWANDISHI posted 4/28/07 8:32 AM    
Wewe unasemaje?
Return To Message Board

http://munishi.com  | Post New Topic