|
Author
|
Topic: Kosoa usitukane ukishindwa funga domo.
|
|
St. Paul
|
posted 11/30/04 6:54 PM
Munishi ndugu yangu sasa naona kazi ya Mungu inaelekea kukushinda. Mimi sina tatizo na kukosoa na kufichua uozo hususani penye lengo la kujenga, lakini mwenendowako si huo. Unachokifanya ni kutukana na kukashifu watu wakiwamo viongozi wa juu wa serikali na madhehebu ya dini. Shutuma nyingi hazina ushaidi wa kutosha, na unazitoa kwa lugha chafu. Kama unatafsiri utandawazi kama uhuru wa kutukana watu bila mipaka jua huo sio utandawazi. Watu wanaheshimu tu huduma ya Mungu ulimojificha ama sivyo ungekuwa ndani wewe. Sasa nakutangazia wazi, kwamba hii na iwe mala yako ya mwisho kutukana viongozi wa nchi yetu kipenzi, na wale wa dini, Usipo fanya hivyo anguko kuu lijuu yako sasa.Jiheshimu nawe utaheshimika.
|
Munishi (Moderator)
|
posted 12/1/04 9:31 AM
Sijatukana na sitarajii kutukana. Kwako matusi ni nini? Kusema CCM iliwaua waislamu zaidi ya sabini Zanzibar, ni matusi? Au kusema Mkapa ndiye anayestahili kuwajibishwa kwani amri ya kuua ilitoka kwake hayo pia ni matusi? Je kusema CCM imezeeka na Watanzania hatuitaki pia hayo ni matusi? Tena kusema CCM OUT.Watanzania wengi wamechoshwa na KERO za CCM. Woga unawafanya waseme wasiyomaanisha.Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. CCM ni Nyani ambaye siku ya kufa kwake imefika. Haijalishi ujuzi wa miaka arobaini kuparamia miti, Lakini safari hii miti yote inateleza. Watapigiza chini kwa kishindo, na ndio mwisho wao. Watanzania tunataka ENZI MPYA bila CCM. Hayo pia ni matusi? Kama kwako hayo ni matusi, basi siombi msamaha, wala sijuti kwa kuwahi kusema hivyo.LIWALO NA LIWE. Hata kufa niko tayari wacha kuwekwa ndani.
|