|
|
|
|
| Author | Topic: CCM WAMEANZA TENA KUUA |
|
Munishi (Moderator) |
posted 11/30/04 2:52 PM
Kana kwamba hawakutosheka na mauaji ya waislamu zaidi ya sabini wakati wa uchaguzi mkuu uliopita,CCM wameanza tena kuua. Safari hii wameanza na kijana mdogo, sijui wataishia wapi.Habari zaidi tunaarifiwa na The Guardian. Angry opposition condemns boy killing Dar Er Salaam 2004-11-30 09:48:54By Peter Tindwa Opposition parties have condemned the police for allegedly killing a 18 year-old pupil, Khalid Omar Mfaume, in Dar es Salaam last Sunday and have formed a probe team. The deceased was among people waiting to cast their votes in the just ended local government elections. Addressing reporters after a meeting of leaders from nine opposition parties yesterday, NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia said the Standard Six pupil at Mbande Primary School, on the city outskirts was gunned down by police at the school grounds. “Political tyranny coupled with use of excessive force have deprived Mfaume of his right to life. His blood will inspire change in this country,” Mbatia said.He warned that ‘dictatorship’ would turn the country into another Rwanda or Kosovo. “We condemn the killing of Mfaume with strongest possible terms,” Mbatia said. A relative of the deceased, Uwesu Seif Magenge, told The Guardian that a group of armed policemen invaded Mbande Primary School and ordered people to disperse. “It was 5pm and many had not cast their votes. They defied the police order. Candidates were ordered to get into a police van. Tension mounted and police opened fire,” Magenge said. But a police statement released at Muhimbili National Hospital where the deceased’s body was preserved alleged that Mfaume died mysteriously. Mbatia told reporters that a four-man team had been formed to establish the cause of the pupil’s death. The team comprises Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa, Fahmy Dugutwa and Khamis Hassan. The four would also work with the family of the late Mfaume in the preparation for the funeral. Leaders who took part in the emergency meeting were from NCCR-Mageuzi, Civic United Front (CUF), FORD, NRA, UMD, NLD, TLP, UPDP and CHADEMA. Meanwhile, opposition leaders have called on the government to repeal the Political Parties Act. “We don’t know what would happen in the general elections next year,” Mbatia said. CUF National Publicity Secretary Tambwe Hiza blamed the Temeke District Commissioner, Baraka Konisaga, for interfering with the voting exercise. “The DC called off polling at National Stadium and seized ballot papers and boxes,” Tambwe charged. He also claimed that the polling station had registered 604 voters but the results indicated that 820 people voted at the National Stadium. CUF National Council would meet on Saturday to assess the civic polls. Both Ilala and Temeke municipal directors John Lubuva and Idi Nyundo respectively declined to comment but promised to announce the results today. In another development, twelve people have been injured in a clash between Morans and villagers during Sunday’s elections, reports Joyce Mkinga. The cause of the fight was not established but eye witnesses told The Guardian that the Morans clubbed voters who were waiting for the polling results at Olopoponyi Village, Njoro Ward. One of those seriously injured, Athuman Hassani, who was hit on his head told The Guardian that some of those assaulted were flushed out of their homes and beaten. According to Hassani, a commotion ensued when results showed that the Maasai candidate, one Makoo Nangolo of CCM, had lost to the opposition. Ten morans were arrested according to Kiteto District Commissioner Lt. Lepillal ole Molloimet.SOURCE: Guardian |
| Mwandishi habari DAR |
posted 12/3/04 2:15 PM
Kweli mzee Munishi mambo huku nyumbani siyo mazuri kabisa. CCM wameanza mchezo mchafu wa kucheza na maisha ya Watanzania. Cha ajabu Polisi wanajaribu kuficha kitu kilicho wazi. Hawataki kutoa ripoti ya kifo huku wakijua wao ndio waliofyatua risasi iliyomuua kijana. SOMENI TAARIFA HII.Sakata la mazishi ya mwanafunzi Khalid Omar Mfaume,limechukua sura mpya kwa ndugu wa marehemu kugoma kumzika wakitaka kwanza wapatiwe ripoti kuhusu chanzo cha kifo chake. Uamuzi huo ulikuja baada ya ndugu kutoridhishwa maelezo ya hati ya kifo ambayo ilisema marehemu amekufa kutokana na kuvuja damu nyingi. Hata hivyo hati hiyo haikusema kiini halisi cha marehemu kuvuja damu nyingi. Uamuzi wa kugoma kuzika maiti hiyo, ulikuja muda mfupi baada ya kuitoa kutoka kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, saa 4:00 asubuhi ya jana. Maiti hiyo ilikuwa mbioni kupelekwa Mbagala kwa mazishi na ilikwishatayarishwa kulingana na taratibu za mazishi ya madhehebu ya Kiislamu. Ilitayarishwa katika msikiti uliopo ndani ya viwanja vya Hospitali ya Muhimbili. Muda mfupi baada ya kumalizika kwa taratibu za kuitayarisha, maiti ilitolewa nje ya msikiti tayari kwa safari ya kwenda Mbagala. Lakini kabla msafara haujaanza, ndugu wa marehemu walitaka wapatiwe ripoti ya uchunguzi wa kifo. Hata hivyo wataalamu waliohusika na uchunguzi huo pamoja na polisi walikataa kuitoa. Kwa upande wao, wataalamu walioifanyia uchunguzi maiti hiyo, walidai kuwa wanaweza kuitoa kama tu kwanza watakuwa wamepata fomu ya PF 9 kutoka polisi. Lakini kwa upande mwingine polisi ilidai kuwa ripoti hiyo inaweza kutolewa tu baada ya miezi mitatu na kwamba kwa sasa inahifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya jeshi hilo. Hali hiyo ilizua mabishano huku ndugu wakisisitiza kuwa ni haki yao kupata ripoti ya kifo cha Khalid. Baadaye ndugu na viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani walikutana kujadili suala hilo. Katika majadiliano yao, walifikia uamuzi wa kuirejesha maiti katika chumba cha maiti, lakini uongozi wa chumba hicho haukutoa ushirikiano. Kitendo hicho kiliwalazimisha ndugu wa marehemu kuamua kuipeleka maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Aga Khan. Ilipofika saa 8:00 msafara wa magari ukiongozwa na polisi uliondoka Muhimbili na kuelekea Aga Khan. Katika hospitali hiyo binafsi, ndugu walipata kibali kilichowawezesha kuingiza maiti ya Khalid katika chumba cha maiti na kuhifadhiwa. Msemaji wa familia ya marehemu, Bw. Yusuf Mbugiro alisema maiti ya Khalid imehifadhiwa ili kutoa nafasi kwao kutafuta wachunguzi binafsi ili waifanyie tena uchunguzi na kwamba ripoti yake itatangazwa hadharani. “Hatutamzika marehemu hadi hapo tutakapojua kiini cha kifo chake…tunashangazwa na kitendo cha polisi na Muhimbili kukataa kusema ukweli kuhusu chanzo cha kifo,” alisema Bw. Mbugiro. Akizungumza na Nipashe, Mwanasheria maarufu, Dk. Sengondo Mvungi alisema kisheria familia ya marehemu ina haki ya kupewa ripoti ya kifo cha ndugu yao. Alisema ni jambo la kushangaza kuona polisi inakataa kutoa ripoti hiyo kwa familia. “Kwa kawaida aliyeomba uchunguzi ufanyike ndiye mwenye haki ya kupewa ripoti…wasipopewa mimi nawashauri wasizike kwa kuwa ni haki yao, “ alisema Dk Mvungi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, alisema alikuwa anawasiliana mara kwa mara na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam , Abdallah Zombe, kumshauri atoe ripoti hiyo. Alisema hata hivyo jitihada hizo hazikuzaa matunda. Na katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limetoa ubani wa Sh 50, 000 kwa familia ya marehemu. Fedha hizo zilitolewa juzi na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salam, Bw. Abdallah Zombe, na zilipokelewa na Mbunge wa Kigamboni (CUF) Bw. Frank Magoba. Bw. Magoba jana alikabidhi fedha hizo kwa familia ya marehemu. Kifo cha Khalid kimekumbwa na utata mkubwa kufuatia kutofautiana kwa taarifa za kiini chake. Kumekuwa na madai kuwa aliuawa kwa kupigwa risasi. Hata hivyo polisi inadai kuwa mwanafunzi huyo alikufa kwa kuchomwa bisibisi. Hali hiyo imeilazimisha familia ya marehemu kuomba maiti ifanyiwe uchunguzi wa kitaalam ili kujua kiini cha kifo. Juzi ulitokea mvutano mkubwa katika ya polisi na ndugu wa marehemu kufuatia kitendo cha polisi kutaka wachukuwe mwili wa marehemu na kuupeleka Mbagala kwa mazishi. Hata hivyo ndugu wa marehemu walipinga kitendo hicho kwa maelezo kuwa Khalid hakuwa mtumishi wa jeshi hilo na wala hakuwa mhalifu. SOURCE: Nipashe |
| JOHO |
posted 12/24/04 1:35 PM
Watanzania tuiombee nchi yetu. Yaliyotokea Rwanda yanainyemelea Tanzania. CCM wanataka kubaki madarakani kwa gharama yeyote, wakati wananchi nao wanasema liwalo na liwe lakini CCM hawaitaki. Sasa asiyekubali kushindwa pengine ndiye mshindani. |
| JOHO |
posted 12/24/04 1:36 PM
Watanzania tuiombee nchi yetu. Yaliyotokea Rwanda yanainyemelea Tanzania. CCM wanataka kubaki madarakani kwa gharama yeyote, wakati wananchi nao wanasema liwalo na liwe lakini CCM hawaitaki. Sasa asiyekubali kushindwa pengine ndiye mshindani. |
|
|