|
Author
|
Topic: ARAFAT AMEKUFA JE ISRAELI ITAPATA AMANI?
|
Munishi (Moderator)
|
posted 11/13/04 9:23 AM
Arafat amekufa. Wapalestina wanaomboleza, Israeli wanashangilia. Ni mapema sana kushangilia. Sharon aliamini kwamba Arafat akifa, amani itainyeshea Israeli kama mvua. Kinyume chake ndio sahihi. Watamkumbuka Arafat japo sasa hawaombolezi kifo chake. Serikali ya Mkapa Tanzania inaamini kwamba Munishi na nyimbo zake ni mwanzo wa kuvurugika kwa amani Tanzania. Kinyume chake ndio sahihi. Amani ilivurugika pale Mkapa alipowaamuru Polisi wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa sababu za kisiasa. Majeshi Tanzania walikasirishwa sana na jambo hilo,na walikuwa tayari kuipindua serikali ya Mkapa. Munishi akaimba wimbo "MPENDE ADUI YAKO", Mkapa badala ajue kwamba wimbo huo ulikuwa ukimsaidia yeye ili serikali yake isipinduliwe na kisha afunguliwe mashitaka ya kuwaua raia wasio na hatia, Aliupiga marufuku wimbo huo na kuamuru polisi wamsake Munishi. Iko siku Mkapa atamkumbuka Munishi. Ngoja kipindi chake cha urais kimalizike, na tunaomba kimalizike salama, halafu Mkapa awe raia wa kawaida. Kombe aliyemwamuru amsake Munishi, ndiye atakayeamriwa amtie Mkapa mbaroni ili ajibu mashitaka ya kuua na kupora mali ya umma pamoja na kuiuza nchi kwa makaburu.
|
Mwandishi wa habari (Moderator)
|
posted 11/16/04 8:42 AM
Nakubaliana nawe kwamba Arafat hakuwa tatizo la Israeli. Lakini mambo yalivyo sasa ni kwamba wale waliokuwa wakitamani kuiangamiza Israeli sasa hawana Arafat wa kuwazuia kufanya hivyo. Ni kweli Israeli watakuja kumkumbuka Arafat.Kuhusu Tanzania, sijui kama kweli Munishi ndiye aliyewashawishi Majeshi Tanzania waache kuipindua serikali ya Mkapa, Lakini kama ni kweli Mkapa anapaswa kumeza kiburi chake na kumshukuru Munishi.Tunayoyasikia hayafai kutoka katika serikali inayoongozwa na aliyekuwa mwandishi wa habari kitaaluma. Mkapa anatuaibisha waandishi habari wenzake barani Afrika.
|
|
Brian kithuku
|
posted 11/29/04 10:18 PM
[This message has been edited on 11/30/2004]
|
|
elisha wa elisha
|
posted 1/4/05 1:50 AM
Kweli Arafat amekufa pamoja na vurugu zake hata kwenye mazishi yake ilikuwa ni vurugu tupu,hivyo Arafat kaenda na UGAIDI wake alivuna alichopanda,hata kama Israel haitapata Amani Arafat alikuwa chanzo cha Ugaidi mashariki ya kati.hata kama dunia itamuunga mkono hawezi kubadilika na kuwa mwanakondoo yeye atabaki kuwa ni Gaidi tu.
|
|
elisha wa elisha
|
posted 1/4/05 1:50 AM
Kweli Arafat amekufa pamoja na vurugu zake hata kwenye mazishi yake ilikuwa ni vurugu tupu,hivyo Arafat kaenda na UGAIDI wake alivuna alichopanda,hata kama Israel haitapata Amani Arafat alikuwa chanzo cha Ugaidi mashariki ya kati.hata kama dunia itamuunga mkono hawezi kubadilika na kuwa mwanakondoo yeye atabaki kuwa ni Gaidi tu.
|