|
Author
|
Topic: Munishi Kaka yangu
|
|
William
|
posted 9/20/04 3:22 PM
Kwa Nd. Munishi,salaam katika jina la bwana wetu Yesu Kristo,Mwanzo wa maisha yako nadhani hukuanza vizuri,lakini baada ya kumpata Yesu maisha yako yalikuwa mazuri ulibarikiwa nasi tulikupenda sana kwa nyimbo zako mahubiri yako na ushuhuda wako. Baada ya muda tukasikia kuwa umekwenda Nairobi kwenye kazi ya Bwana. Lakini tunavyoona kwa sasa UPAKO UMEONDOKA KWAKO.Kwa sababu web site yako imejaa malumbano kuliko kumwinua Yesu Kristo. Well its not bad kuwa sehemu ya siasa, that's nice and good, you can just do both, no problem, but it depend on the way you do that, we all know respect ambayo Mwl Nyerere ameiletea nchi, na kwa sehemu amefanya vizuri.If you want to be a party of politics, is fine brother, but see the right ways to do it, don't raise yourselves. Brother don't rush unto things, get them in details please. Uwe umetulia, have time with God, pray and stay in his presence, that's all.As I say its not bad for a christian to do something politics, but you don't do compaign like them, not if God wants you to be a leader for his people or Nations, you will, don't go ahead and leave God behind, NO! NO! NO!Achana na haya mambo hayatakusaidia kitu, wewe hubiri Injili, sasa umeanza mpaka kusema watumishi kama Kulola na wengine, well hata kama wanafanya makosa, don't point out makosa yao, waombee, that's all.Don't see them, just see the devil behind them, please restore your respect brother, I never knew you in details than a good Man of God, and I always want it to be that way.Tulikuwa tunapenda sana huduma yako ya uimbaji na ushuhuda wako lakini kwa sasa hatuoni mfano, kwa kweli hapo hatuna lakujifunza kutoka kwako. Ninonavyo mimi na wenzangu ni HERI UMUHUBIRI YESU KRISTO UMWINUE YEYE NAYE ATAKUINUA. UMUTUKUZE YEYE NA KUMSIFU KAMA HAPO MWANZO NAWE UTABARIKIWA KAMA HAPO MWANZO. KWA SASA SISI TUNAONA UMEICHA NJIA. VITA VYETU SISI NI VYA KIROHO.UPAMBANE NA SHETANI SIYO MTU!!!!
|
|
Munishi
|
posted 11/2/04 9:23 AM
Sawa. Huo ni mtizamo wako, ambao unahitaji maelezo kutoka kwangu. Mimi sijaacha kuihubiri Injili. Kama kuna wakati ninapoihubiri injili kwa ujasiri ni sasa. Kukemea, Kukaripia, Kuonya na kufundisha, ni sehemu ya injili. Kuombea wengine pia ni INJILI.Sasa nimekjosea wapi kuwakemea kina Mkapa wauaji, wezi wa mali za umma? Unataka niwaombee? Hawajakubali makosa yao na kutubu. wakifanya hivyo nitawaombea. Uniombee nipate ujasiri wa kuwakemea hasa wale wanaomwabudu Marehemu Nyerere. Alifanya mazuri kwa mtizamo wako, wacha tuseme mabaya yake kwa mitizamo yetu tulio wengi. Ikiwa hamtaki kuyasikia mabaya yake, kwa nini mtuambie mazuri yake? Acheni unafiki.
|
|
Brian kithuku
|
posted 11/29/04 9:30 PM
Kwa kweli bwana Munishi huku Tanzania tumechoshwa na matusi yako. Nakutahadharisha, usirudi kabisa huku, baki huko huko Kenya. Kwa matusi unayotukana na hasira uliyotusababishia ukionekana Tanzania watu wanaweza kukutafuna mzima mzima. Mtu huna hata haya!
|
|
amani
|
posted 11/30/04 3:11 PM
Katika watu amabao jamii ya Tanzania inahitaki kuwaangalia kwa makini wewe ni mmoja wao kaka Munishi. Binafsi na waliowengi tuliridhiswa na kazi zako katika kutangaza injili. Ghafla mwenzetu umekurupuka kutoka huko uliko na kuona kila kilichopo Tanzania ni uozo. Nani kakupa elimu hiyo? Ninani aliye kuroga hata ukaona Kenya na kwingineko kuna wema zaidi kuliko viongozi wetu wa juu? Ni imani na wokovu gani unakupa wewe kibali cha kuwa juu ya mamlaka. Kwa taarifa yako, kama wewe umechoka na Tanzania, sisi tunaizimia mno, na hatufikirii kuihama jama nje tunatoka sana vile vile. Kama wewe unakipawa cha kukemea, Mkemee na kumtukana Mzee, Rais Kibaki anapokwenda kombo uone moto unakuvyokuwakia. Hufanyi hivyo sababu huko umepewa hifadhi. Sasa wataka mambo yetu yachafuke huku halafu ufurahi tutakuwa tunakuja huko kama wakimbizi ausiyo.Hujatulia babke, na wala roho wa Mungu sasa hakuongozi katika mambo fulani. Uchambuzi, uchanganuzi na upembuzi yakinifu wa masuala ya siasa, uchumi na dini unahitaji elimu yakutosha, ufahamu na upeo wa juu katika masuala ya kitaifa na kiulimwengu. Upeo wako bila shaka ni mdogo.Nakushauri umrudie Mungu kisha itafute elimu na uikamate wala usiiache iende zake. Siasa zetu kwa taarifa yako ni bomba sana, pamoja na mapungufu makubwa tunayoyaona kila siku.Jema ni kwamba serkali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo kwa ajili ya watu wote, na iko tayari muda wote kurekebisha udhaifu wowote kwa utaratibu muafaka. Kama kuna mwanafalsafa ambaye tunapashwa kujivunia Tanzania, wakwanza ni Mwalimu Nyerere. Kama unapenda kuangalia udhaifu wake, kumbuka yeye hakuwa malaika. Alifanya kila awezalo kuboresha maisha ya wengi. Tuambie ungekuwa wewe ungetufanyia nini zaidi ya Nyerere? Kama huna habari, Rais Mkapa ni mmoja kati ya wachache ambao wameweza kuendesha nchi katika hali ngumu kiuchumi bila kuteteleka.Sasa kama kila kitu cha Bongo unakiona feki, tuachie Bongo yetu vilivyo vyetu,na maswala ya Gospel wachie wanaoyaweza ili usimtukanishe Aliye juu. Hujatulia.
|